Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema uamuzi wa Mkutano Mkuu CCM kupitisha majina ya wagombea urais wawili Rais Dk Hussein Ali Mwinyi kumethibisha kuwa Makmau Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Ismail Jussa Ladhu ni kiongozi mropokaji .
Chama hicho kimewataka wazanzibari kupuuza porojo, uongo na uzandiki anaoutumia Jussa kwenye mikutano ya hadhara ya chama chake .
Akijibu swali aliloulizwa na Waandishi wa habari jijiji Dodoma baada ya kumalizika mkutano mkuu ,walitaka kujua iwapo Rais Dk Mwinyi atamshinda mgombea urais wa ACT Wazalendo na Makamo wa kwanza wa Rais SMZ, Othman Masoud Othman.
Mbeto akijibu swali hilo , alisema kupitishwa majina mawili ya Rais Dk Samia Suluhu Hasaan na mwenzake Rais Dk Mwinyi ni baada ya kuonyesha uwezo wa kiutendaji wa serikali zao zinavyotumikia nchi na wananchi.
Alisema kwa zanzibar Wajumbe wa Mkutano Mkuu kwa uamuzi mmoja , wameridhishwa na uchapakazi wa Rais Dk Mwinyi , utekelezaji na utendaji wa kisera chini ya ilani uchaguzi ya CCM mwaka 2020/2025.
“Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa ndio walioshinikiza uteuzi wa wagombea urais ufanyike. Wamevutiwa na uchapakazi wenye ufanisi katika maendeleo ya kisekta.Dk Samia na Dk Mwinyi wamevunja rekodi” Alisema Mbeto.
Pia Katibu huyo Mwenezi alisema uamuzi huo wa wajumbe, umemfedhehesha Jussa na kuthibitisha matamshi yake ni ya mwanasiasa kizabizabina, lipyoto , kiongozi asiyefaa na mropokaji .
“Jussa amefedheheka kwa uzushi wake .Alidai Rais Dk Mwinyi anapingwa ndani ya CCM .Akasema hatateuliwa kuwania urais. Kamuulizeni Jussa ni kina nani waliopitisha jina la Dk Mwinyi kwa kishindo? ” Alihoji Mbeto
Aidha alimtana Jussa ni Mwanasiasa asiyekijua vyema CCM hivyo atapata taabu sana huku akishuhudia CCM kikiendelea kushindana chaguzi zote kidemokrasia kwa ustadi wa sera zake.
Akimuelezea Makamu huyo Mwenyekiti wa ACT, Mbeto alimtaka Jussa kuwaeleza ukweli wanachama wa ACT ,midhali Hayati Maalim seif Sharif Hamad hakuiweza CCM , Othman hana ubavu wa kumshinda Dk Mwinyi
‘Kwa kazi kubwa iliofanywa na Rais Dk Mwinyi ya kuleta mageuzi ya kimaendeleo Zanzibar. Upinzani hauwezi kuambua lolote . Wananchi si wajinga wa kupuuza mema yanayoonekana na kuendelea kuamini ahadi za uongo na porojo za Jussa “Alieleza
Hata hivyo Mbeto alisisitiza CCM kitashinda chaguzi zote kuu Tanzania na Zanzibar kutokana na watanzania wengi kuziamini sera za chama hicho ambazo zinahimiza umoja,amani na utulivu.