Uzinduzi wa Hotel ya Hyatt Regency Kuongeza Uchumi na Utalii wa Kenya

Katika hatua muhimu kwa sekta ya
utalii na uchumi wa Kenya, Hyatt Hotels Corporation rasmi imezindua
hoteli yake ya kwanza katika nchi hiyo, Hyatt Regency Nairobi Westlands,
mapema hii leo. Huku ikiwa katika eneo lenye shughuli nyingi la
Westlands, hoteli hiyo yenye hadhi ya nyota tano inatarajiwa kuboresha
si tu utalii bali pia fursa za biashara katika eneo hilo, hivyo
kuimarisha hadhi ya Nairobi kama mahali bora pa kusafiri kwa ajili ya
burudani na shughuli za kibiashara.


Hyatt
Regency Nairobi Westlands, iliyo na vyumba 219, inakusudia kukidhi
mahitaji yanayoongezeka kutoka kwa wasafiri wa biashara na watalii kwa
pamoja, huku ikijipambanua kama eneo kuu la mikutano na matukio. Huku
ikiwa na anuwai ya vifaa na kuzingatia kutoa uzoefu wa kipekee wa
ukarimu unaounganisha vipengele vya kitamaduni na viwango bora vya
huduma hoteli hiyo inatarajiwa kuvutia watalii wa ndani zaidi huku
ikisaidia uchumi wa eneo hilo.

Stephen
Ansell, Mkurugenzi Mtendaji wa Hyatt kanda ya Mashariki ya Kati na
Afrika, alionesha furaha kuhusu uzinduzi wa hoteli hiyo, akisema, “Huu
ni mwanzo wa hatua muhimu katika mkakati wa ukuaji wa Hyatt barani
Afrika. Tumejitolea kupanuka kwenye maeneo yanayovutia, kuhakikisha kuwa
mahitaji mbalimbali ya wasafiri wa kisasa yanakidhi mahitaji,
tunapowapa wanachama wa Dunia ya Hyatt na wateja zana zaidi za
kuchagua.”

Hoteli hii
si tu ongezeko kwenye mandhari ya Westlands; inatarajiwa kuwa kitovu hai
cha shughuli mbalimbali. Wageni katika Hyatt Regency Nairobi wataweza
kufikia kwa urahisi baadhi ya vivutio maarufu vya nchi hiyo ikiwa ni
pamoja na Makumbusho ya Kitaifa ya Nairobi, Msitu wa Karura, na Hifadhi
ya Taifa ya Nairobi, ambavyo vyote vinaangazia utajiri wa asili na
kitamaduni wa Kenya. Ukaribu na vituo vya manunuzi kama Sarit na
Westgate Mall pia unaiweka hoteli hii kama kitovu rahisi kwa wageni
wanaotaka kujiunga na mambo ya kitamaduni na ya kisasa ya Kenya.

Igor
Jovovic, Meneja Mkuu wa Hyatt Regency Nairobi Westlands, alisisitiza
dhamira ya hoteli hiyo kutoa uzoefu wa kweli wa Kenya, akisema, “Tangu
muundo wetu unaoonyesha mandhari yenye rangi nyingi za Kenya hadi milo
yetu iliyopangwa kwa ustadi, Hyatt Regency inalenga kuwakilisha ladha
bora za Kenya. Uzoefu wa aina hii ni muhimu kwa watalii wanaotafuta
kuungana na utamaduni wa eneo hilo, na hatimaye kuhimizia kukaa kwa muda
mrefu na kutembelea tena.’’

Hoteli
yenyewe imeundwa kukidhi mahitaji ya aina mbalimbali ya wageni, ikiwa
na muunganiko wa vyumba 147, suites, na apartments 72. Imejaa vifaa vya
kisasa kama vile Wi-Fi ya kasi, TVs za kisasa, na miundombinu ya kuogea
ya kifahari.

Mbali na
malazi yake ya kifahari, Hyatt Regency Nairobi Westlands inatoa uzoefu
tofauti wa vyakula, ukichanganya ladha za ndani na vyakula vya
kimataifa, ambayo yanatarajiwa kuvutia wapenda chakula. Aidha, anuwai ya
vifaa vya hoteli hiyo ni pamoja na kituo cha mazoezi chenye teknolojia
ya kisasa, studio ya mazoezi ya aerobic, na bwawa la kuogelea la ndani
linaloonesha mandhari nzuri ya jiji, likifanya kuwa mahali bora kwa
kupumzika na burudani.

“Wasafiri
wa biashara wataona maeneo ya mikutano ya hoteli hii yenye mvuto wa
kipekee. Gorofa ya juu ina moja ya ballroom kubwa zaidi barani Afrika
Mashariki, ikitoa mandhari nzuri ya jiji na nafasi kubwa ya matukio
makubwa na mikutano. Kwa zaidi ya futi za mraba 21,520 zilizotengwa kwa
aina mbalimbali za mikutano, ikiwa ni pamoja na maeneo kumi tofauti
yenye teknolojia ya kisasa ya sauti na video, hoteli hii imejiandaa
kushughulikia mikutano ya kibiashara iliyo na hadhi kubwa,” aliongeza.

Stephen Ansell, Mkurugenzi Mtendaji wa Hyatt kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika.


Igor Jovovic, Meneja Mkuu wa Hyatt Regency Nairobi Westlands

Related Posts