Dar es Salaam. Matokeo ya jumla ya uchaguzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), yametangazaa huku Tundu Lissu akiibuka kidedea.
Katika nafasi hiyo ya Mwenyekiti wa Chadema Taifa, wapigakura waliojisajili walikuwa 1,014 kura zilizopigiwa ni 999, halali zikiwa 996 na tatu zimeharibika.
“Odero Odero kapata kura moja sawa na asilimia 0.1, Freeman Mbowe amepata kura 482 sawa na asilimia 48.3 huku Lissu akipata kura 513 sawa na asilimia 51.5,” amesema Profesa Raymond Mushi mwenyekiti wa uchaguzi.
Nafasi ya Makamu mwenyekiti wa Chadema Zanzibar ameshinda Said Mzee Said ambaye amepata kura 625 sawa na asilimia 89 ya kura 706 huku halali zikiwa 700 na sita zimeharibika.
Katika upande wa Makamu mwenyekiti bara idadi ya wapigakura ni 1, 014 zilizopigwa ni 1005, halali zikiwa 998 na saba zimeharibika.
Hivyo, Matharo Gegul alipata kura 49 asilimia 5, Ezekia Wenje (kura 372, sawa asilimia 37), John Heche na kura 577 sawa na asilimia 57. Hivyo Makamu mwenyekiti wa Chadema bara ameshinda Heche.
Uchaguzi huo umesimamiwa na wazee wanane akiwamo Profesa Mushi na Katibu akiwa Dk Azaveli Lwaitama. Wengine ni Ruth Mollel, Ahmed Rashid, Alfred Kinyondo na Azumuli Kasupa.
Endelea kufuatilia Mwananchi