WAANDISHI WASAIDIZI NGAZI YA KATA KUTOKA MASASI, NANYUMBU WANOLEWA

Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Dkt. Zakia Mohamed Abubakar leo Januari 22,2025 ametembelea mafunzo kwa Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata katika Halmashauri ya Masasi Mji na Masasi DC mkoani Mtwara na kushuhudia washiriki hao wakifanya mafunzo kwa vitendo. Mafunzo hayo ya siku mbili yalianza Januari 21 na kumalizika Januari 22, 2025.

Mafunzo hayo ni maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotaraji kuanza Januari 28, 2025 na kufikia tamati Februari 03,2025 ambapo vituo vitafunguliwa Saa 2:00 asubuhi na kufungwa Saa 12:00 jioni.

Afisa Mwandikishaji wa Halmashauri ya WSilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara, Ndg.Juma Njaro akifungua mafunzo ya siku mbili leo Januari 21,2025 kwa Maafisa Waandikishaji Wasaidizi ngazi ya Kata yanayofanyika kwenye ukumbi ukumbi wa Halmashauri hiyo.

Mafunzo hayo ni maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linalotaraji kuanza Januari 28, 2025 na kufikia tamati Februari 03,2025 ambapo vituo vitafunguliwa Saa 2:00 asubuhi na kufungwa Saa 12:00 jioni.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo hayo, Njaro aliwataka waandishi hao wasaidizi ngazi ya Kata kuzingatia mafunzo kwani wanaenda kuwafundisho waandishi wasaidizi ngazi ya vituo na waendesha vifaa vya Biometriki (BVR) vituoni wakati wa zoezi.

Afisa Uhamiaji wa Wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara, Mrakibu wa Uhamiaji Hendrick Mtui akiwasilisha mada kwa washiriki wa Halmashauri ya Nanyumbu kuhusu uraia na nani ni raia wa Tanzania.

Washiriki wakifuatilia mada wakati wa mafunzo hayo.

Maafisa Waandikishaji wasaidizi ngazi ya Kata kutoka Halamashauri ya Wilaya ya Nanyumbu jimbo la Nanyumbu Mkoani Mtwara wakila viapo vya kujitoa uanachama wa chama cha siasa na kutunza siri mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Nanyumbu, Mhe. Asifiwe Crispo Jembe, muda mfupi kabla ya kuanza kwa mafunzo ya siku mbili yaliyoanza leo Januari 21,2025 na kumalizika kesho Januari 22,2025 kuhusu uboreshaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura.

Washiriki wakiwa mafunzoni.

Related Posts