Waliozuiliwa matokeo kidato cha nne kurudia mitihani 2025

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limezuia matokeo ya wanafunzi 459 wa kidato cha nne mwaka 2024 kwa sababu mbalimbali zilizosababisha wasifanye mitihani yote.

Hata hivyo wanafunzi hao wamepewa fursa ya kurudia mitihani ya kidato cha nne mwaka huu 2025.

Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Dk Said Mohammed, akitangaza matokeo ya kidato cha nne leo Alhamisi Januari 23, 2025 amesema wanafunzi hao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mitihani ya kidato cha nne kwa masomo yote au idadi kubwa ya masomo.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Related Posts