Ajali ya bodaboda yamtibulia Ngalema

BEKI wa Tanzania Prisons, Paul Ngalema amesema sababu ya kutoonekana na timu hiyo tangu asajiliwe msimu huu anauguza majeraha ya ajali ya bodaboda aliyopata Julai mwaka 2024, mkoani kwao Dodoma.

Ngalema kabla ya kuripoti kambini (Prisons) katika mizunguko yake alipanda usafiri wa bodaboda, akashangaa ghafla mbele yao kuna  magari mawili, kitendo cha kutaka kujiokoa akuruka na kujikuta amepata majeraha nyuma ya kisigino.

“Baada ya kwenda hospitali niliambiwa kuna mshipa nyuma ya kisigino kwa kitaalamu ni achilles tendon paliachia sentimina nne, hivyo nikafanyiwa upasuaji nikaambiwa nipumzike miezi tisa, nikauomba uongozi wa Prisons nijiuguze nikiwa nje ya kambi, hivyo nitaungana nao msimu ujao,” alisema Ngalema na kuongeza;

“Zilikuwa nyakati ngumu kuumia nje ya timu na kabla ya kuanza kuitumikia, sikuwa na namna ya kukabiliana na hilo, kwa sasa nafanya mazoezi mepesi ili kurudi katika hali yangu ya kawaida.”

Prisons ilimsajili mchezaji huyo kutoka Dodoma Jiji chini ya aliyekuwa kocha wao Mbwana Makata.

Related Posts