Uhamiaji yafafanua nyota Singida BS kupewa uraia Tanzania

Idara ya Uhamiaji imethibitisha kwamba wachezaji watatu wanaocheza Singida Black Stars, Emmanuel Kwame Keyekeh (Ghana), Josephat Arthur Bada (Ivory Coast) na Mohamed Damaro Camara (Guinea) wamepewa uraia wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Uhamiaji ni kwamba Keyekeh, Bada na Camara waliomba na kupewa uraia kwa mujibu wa vifungu vya 9 na 23 vya Sheria ya Uraia ya Tanzania, Sura ya 357.

“ldara ya Uhamiaji inapenda kutoa ufafanuzi wa taarifa zilizochapishwa na kujadiliwa kwenye mitandao ya kijamii na Vyombo vya Habari kuhusu kupatiwa uraia wa Tanzania wachezaji watatu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Singida Black Stars. Wachezaji wanaotajwa kwenye taarifa hizo ni kama ifuatavyo:-

1.Emmanuel Kwame Keyekeh (Ghana),

2.Josephat Arthur Bada (Cote d’Ivoire), na

3.Muhamed Damara Camara (Guinea).

“Wachezaji tajwa waliomba na kupewa uraia kwa mujibu wa vifungu vya 9 na 23 vya Sheria ya Uraia ya Tanzania, Sura ya 357.

“Kwa muktadha huo, Idara ya Uhamiaji inapenda kuutaarifu Umma kuwa watajwa ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi,” ilieleza taarifa hiyo iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, SSI. Paul J. Mselle.

Related Posts