MSHAMBULIAJI wa JKT Tanzania, Charles Ilanfya juzi Jumanne ameanza mazoezi ya gym tangu alipoumia Agosti 28 timu hiyo ilipocheza dhidi Azam FC katika Uwanja wa Major Generali Isamuhyo.
Katika mchezo huo Ilanfya aliangukia goti bila kusukumwa na mtu, kisha likaanza kuvimba na baada ya kwenda hospital aliambiwa anatakiwa kukaa nje msimu mzima.
“Goti lilivimba sana na baada ya kupelekwa hospital na viongozi wa timu, daktari aliniambia nianze kwanza kutumia dawa ili uvimbe upungue, ndipo viendelee vipimo vingine.
“Baada ya hapo nikafanyiwa upasuaji wa goti la mguu wa kulia, ilinibidi nikae kwa muda mrefu nje na sasa daktari ameniambia nianze mazoezi ya gym.”