Shule ya Kimataifa ya Al-Irshaad yakuza vipaji

-Vijana wake wa Mpira wa miguu kumenyana  na Tottenham na Wolves

Shule ya Kimataifa ya Al-Irshaad iliyopo Masaki Jijini Dar es Salaam inawataka Watanzania kupeleka watoto wao kupata elimu shuleni hapo ili kuvumbua na kuendeleza vipaji vya vijana wa Kitanzania.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Salim Sadiq anasema swala la kukuza vipaji na kuviendeleza ni la kipaumbele kwani katika Ulimwengu wa sasa vipaji vinalipa na kuchangia pato la Taifa.

“Unaona wachezaji wakubwa mpira wa miguu, riadha hata kuogelea wanavyoingiza pesa nyingi kutokana na vipaji vyao na hivyo kuchangia pato la taifa , sasa sisi hapa ndipo mahala pake pa kusaidia vijana wenye vipaji kufikia malengo yao.

Mkuu huyo wa shule anasema shule hiyo inafundisha masomo yake kwa mtaala wa Cambridge na hivyo kuwapa vijana fursa kupata elimu bora kuanzia Shule Msingi hadi Sekondari Darasa la Tisa.

Wanafundisha pia masomo ya Dini ya Kiislam, Lugha ya Kiarabu na Quran tukufu , lengo ni kujenga taifa lenye maadili mema.

Kuhusu masomo ya ziada Mkuu huyo wa shule anasema kwamba kuna club mbalimbali za vijana kama Kuogelea, Mpira wa Miguu, Karate na fani mbalimbali za kazi za mikono mfano mapishi na kushona.

Masomo yanalenga kuwafanya vijana kijitegemea sababu yameegemea zaidi katika vitendo kuliko nadharia.

Timu ya Mpira wa miguu iko mbioni kwenda Uingereza kucheza na washirika wao klabu maarufu za soka nchini humo za Tottenham na Wolverhampton , wana waalimu wa daraja la juu katika fani zote.

Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Salim Sadiq

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Kimataifa ya Al-Irshaad iliyopo Masaki Jijini Dar es Salaam

Related Posts