Katibu Mkuu wa UVCCM, Jokate Mwegelo, amepongeza wanafunzi, walimu, na uongozi wa Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani, kufuatia mafanikio makubwa ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jokate Mwegelo Girls katika matokeo ya kidato cha nne.
Shule hiyo imepata ufaulu wa juu kwa daraja la kwanza (division one) 73, daraja la pili (division two) 9, daraja la tatu (division three) 4, huku kukiwa hakuna division four wala zero.
Shule hiyo ilipewa jina la Jokate wakati alipokuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, ambako alianzisha kampeni ya “Tokomeza Zero” iliyofanikiwa kwa kiasi kikubwa, ikiwemo kuendesha harambee iliyowezesha ujenzi wa shule hiyo.
Jokate alisema: “Wow, hizi division one si za kawaida! Mabinti wetu wamefanya kazi kubwa kwa kuwa huu ni mtihani wao wa kwanza. Hongereni sana! Pia tunawapongeza uongozi wa Kisarawe na Mkoa wa Pwani kwa kuendelea kufanikisha kazi hii kwa viwango vya juu, hasa Mbunge wangu wa Jimbo la Kisarawe, Jafo.”