TAWA IMESHIRIKI WIKI YA SHERIA KANDA YA DAR ES SALAAM


MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA) Kanda Maalum ya Dar es Salaam imeshiriki katika maandamano ya kuanzishamisha wiki ya sheria
Maandamani hayo yameanzia Mahakama Kuu, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuhitimishwa katika viwanja vya mnazi mmoja huku yakishirikisha wahifadhi kutoka Makao Makuu ya Kanda na kituo cha Magofu leo januari25,2025.
Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ilikuwa ni’Tanzania ya 2050,Nafasi ya Taasisi zinazosimamia haki,madai katika kufikia malengo Makuu ya dira ya Taifa ya Maendeleo’
Akimuwakilisha Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila, Mkuu wa wilaya ya Temeke Sixtus Mapunda amewaomba wananchi kuishi katika hali ya amani na utulivu ili kupunguza kesi mbalimbali zinazojitokeza katika jamii.
Kamishna wa Uhifadhi (TAWA) akiwakilishwa na Kamanda wa Uhifadhi Kanda Maalum Dar es Salaam,Twaha Twaibu amesema Mamlaka hiyo imeshiriki maadhimisho ya wiki ya sheria ili kuwajengea uwezo wananchi wa kutambua sheria mbalimbali zinazoharamisha kufanya mawindo kwenye mapori .
“Wananchi wanaweza kudhani ni haki yao kuwinda mnyama kwa kuwa yupo porini lakini ni kinyume cha sheria taratibu zipo nasi leo tutakuwa na wajibu wa kuwaelekeza wananchi wakitaka kufanya mawindo yapo maeneo yametengwa kisheria ni vyema wakauliza kwenye mamlaka za vijiji vyao pamoja na ofisi zetu” amesema Twaibu.
Twaibu amesema kuwa Mamlaka hiyo imepambana kuondosha ujangiri “mmeona matokeo ya kudhibiti ujangiri kule vijiji mmesikia Tembo jinsi wanavyozaliana wamekuwa wengi “, amesema Twaibu.
Amesema Mahakama ni sehemu muhimu katika mchango wa kudhibiti matendo ya ujangiri hivyo wao ni wadau muhumu wa mahakama hivyo maadhimisho hayo yatumike kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuwalinda Wananyama pori.

Afisa Mahusiano wa Tawa kutoka Kanda maalum ya Dar es Salaam,  Twaha Twaibu akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza matembezi ya ufunguzi wa wiki ya sheria nchini yaliyoanzia katika Viwanja vya Mahakama kupitia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuhitimishwa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.

Related Posts