RUWASA YATAMBULISHA MRADI WA MAJI WA WANANCHI NYASA

Na Mwandishi Wetu, Nyasa

WAKALA wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma, umetambulisha kwa Wananchi mradi wa maji wenye thamani ya zaidi ya Tsh Milioni 962.7 unaokwenda kutekelezwa katika vijiji viwili vya Lumeme na Mbanga ili kutatua kero ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na Salama katika Vijiji hivyo.

Mradi huo umetambulishwa kupitia mkutano ya hadhara uliofanyika katika viwanja vya Ofisi ya Serikali ya kijiji cha Mbanga kwa lengo la kuwashirikisha Wananchi, ili waweze kushirikiana na Mkandarasi atakayetekeleza Mradi na kuhudhuriwa na wananchi, Viongozi wa Chama na Serikali.

Akizungumza na Wananchi wa kijiji hicho Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Peres Magiri, amemtaka Mkandarasi anayetekeleza Mradi, kuhakikisha anajenga mradi kwa ubora na ukamilike kwa wakati na kuhakikisha maji yanatoka ili kuwaondolea Wananchi adha ya ukosefu wa huduma ya maji kwenye maeneo yao.

Magiri alisema, Serikali imekusudia kutatua kero ya maji, hivyo mradi huo ni lazima uendane na gharama halisi ya fedha zilizotengwa na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwenye utekelezaji wa mradi kwa kulinda vifaa vitakavyoletwai na kutunza vyanzo vya maji ili mradi uwe endelevu.

“Mkandarasi uliyepewa kazi ya kutekeleza mradi huu,hakikisha unajenga kwa ubora na maji yanatoka, Serikali imetenga fedha nyingi ili kutatua kero ya maji kwa Wananchi wake pia, Wananchi naomba tushiriki kikamilifu katika Ujenzi wa mradi huu kwa kuwa ni wenu”alisisitiza Magiri.

Awali Meneja wa RUWASA Wilayani Nyasa Mhandisi Masoud Samila alisema mradi utatekelezwa na Mkandarasi Mzawa Kampuni ya CONSEL CONSTRUCTION AND ENGINEERING SERVISES CO.LTD Kutoka Mwanza na wamejipanga kikamilifu kusimamia na kutekeleza mradi ili uweze kukamilika kwa wakati na kutatua changamoto ya upatikanaji wa maji safi kwa wananchi wa vijiji hivyo.

Alisema, Mradi unalenga kuhudumia wananchi wapatao 4,990 na vijiji vitakavyonufaika na mradi huo ni Mbanga na Kigongo na utakapokamilika utapunguza magonjwa ya mlipuko na kutoa huduma ya maji safi na salama kwa Wananchi na kuongeza muda wa kufanya kazi za kujiletea maendeleo.

Ametaja kazi zitakazofanyika ni ujenzi wa mtego wa maji,ujenzi wa Tanki lenye ujazo wa Lita milioni Moja(150,000),ununuzi wa Bomba, ulazaji wa mabomba km 32, ulazaji w bomba kuu Km.1 ujenzi wa vituo 10 vya kuchotea maji na muda wa utekelezaji wa mradi ni miezi sita na unatarajia kukamilika tarehe 6 April mwaka huu.

Samila,ametoa wito kwa Wananchi kushirikiana na Mkandarasi anayetekeleza mradi ambaye tayari ameshaanza kazi na yuko eneo la mradi ili aweze kukamilisha kazi kwa wakati uliopangwa.

Wananchi wa vijiji hivyo kupitia Mbunge wa Jimbo la Nyasa Stella Manyanya wameipongeza Serikali ya awamu ay sita kwa kutatua changamoto ya maji kwenye vijiji vyao kwani kwa muda mrefu hawana maji safi n salama.
.
Naye Mbunge wa Jimbo la Nysa Mhandisi Stella Manyanya alisema, Serikaliya Chama cha Mapinduzi inaendelea kutatua Kero mbalimbali za Wananchi na kuwataka wananchi kuendelee kuwa na imani na Serikali na kuiunga mkono katika kutekeleza miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa lengo la kuboresha maisha na kukuza uchumi wao.
 

Meneja wa RUWASA Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma Masoud Samila kulia,akimkabidhi Mkuu wa Wilaya hiyo Peres Magiri Mkatabata wa ujenzi wa mradi wa maji unaotekelezwa katika vijiji viwili vya Mbanga na Lumeme ili kumaliza kero ya huduma ya maji safi na salama kwa Wananchi.
 

Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Mbanga Wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma,wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo Peres Magiri(hayupo pichani)wakati wa hafla fupi ya kutambulisha mradi wa maji unaotekelezwa na Serikali kupitia Wakala wa maji  na usafi wa mazingira vijijini(RUWASA) ili kuwaondolea Wananchi kero ya upatikanaji wa huduma ya maji.
 

Mkuu wa wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma Peres Magiri,akizungumza na Wananchi wa kijiji cha Mbanga kabla ya kutambulisha mradi mkubwa wa maji unaotekelezwa katika kijiji hicho.

Related Posts