Presha ya mchezo wa Tabora United dhidi ya Simba inazidi kupanda mdogondogo na taarifa ya kushtua ni kwamba mchezo huo utaamuliwa na mwamuzi Amina Kyando ambaye hana rekodi nzuri na wenyeji wa mechi hiyo.
Kyando ataamua mechi hiyo ya tatu kwenye historia ya Tabora United huku mechi mbili zilizotangulia akikumbana na matukio ya utata yaliyosababisha kufungiwa.
Kyando kutoka Morogoro atasaidiwa na Robert Luhemeja na Fatma Mambo kuamua mchezo huo utakaopigwa Jumapili Februari 2 katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora.
Kwenye mechi mbili ambazo Kyando ameziamua dhidi ya Biashara United iliyopigwa Juni 12,2024 alitoa penalti iliyozusha utata wakati wa mchezo wa kuamua timu ipi ipande Ligi Kuu au kubaki Championship.
Penalti hiyo iliyotolewa dakika ya 90+7 kati ya dakika 9 za nyongeza ndio iliamua mchezo huo ambapo hata hivyo kwenye mchezo wa marudiano Tabora iliibuka na ushindi ulioibakisha Ligi Kuu.
Mchezo mwingine ulikuwa dhidi ya Simba msimu uliopita wa kumalizia msimu, ambapo Kyando alikataa bao la Tabora United lililofungwa kwa shuti kali na aliyekuwa kiungo wa timu hiyo, Najim Mussa.
Hata hivyo, uamuzi huo uliofanyika Mei 6, 2024 katika Uwanja wa Azam Complex, Simba ilishinda kwa mabao 2-0 yalisababisha baadaye mwamuzi huyo kufungiwa.
Kyando anakwenda kuchezesha mechi ya tatu dhidi ya Tabora United, huku akiwa hana kumbukumbu nzuri dhidi ya wauza asali hao.