Na Jane Edward, Arusha
Naibu Mkurugenzi Mtendaji uzalishaji umeme kutoka Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) Mhandisi,Costa Rubagumiya amesema Tanzania inampango wa kuwapatia wananchi milioni 8. 3 umeme kufikia mwaka 2030.
Costa ameyasema hayo leo wakati wa Mkutano wa nishati wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki (EAECS) uliofanyika jijini Arusha.
Amesema kuwa mkutano huo unalengo la kuhamasisha ufikiaji wa wananchi katika uzalishaji wa umeme, usafirishaji , usambazaji hadi kwa watu ambao gridi za umeme hazijawafikia .
Aidha amesema ni lazima benki kama Stanbic na nyinginezo kuweka mazingira mazuri ya biashara ili kuvutia wawekezaji katika sekta ya nishati.
Amefafanua kuwa Tanesco inawaunga wateja laki tano kila mwaka hivyo imejiwekea malengo mapya ya ongezeko la wateja na kufikia milioni 1.6 hadi kufikia mwaka 2030.
Alisema kisiwa cha Mafia na vinginevyo vilivyopo Ziwa Victoria maeneo hayo lazima wawekezaji tuwavutie na kuwekeza zaidi katika bei ambayo wananchi wataimudu na serikali imeweka mazingira mazuri kuhakikisha wawekezaji hao watakapoanza kazi wanakuwa katika mazingira mazuri ikiwemo wananchi kunufaika.
Jean Baptiste Havugimana ni Mkurugenzi wa uzalishaji kutoka Jumuiya ya Afrika mashariki ambapo anasema mahitaji ya nishati ya umeme ni makubwa katika nchi za EAC na kwamba mikakati ni kuhakikisha umeme wa uhakika unapatikana.
“nia ya mikutano hii ni kuona nchi hizo zinaondokana na giza ili kuweza kuwezesha sekta mbalimbali ikiwemo viwanda wanazalisha bidhaa zao bila kupata usumbufu wa mgao wa umeme ambao umekuwa ukizikumba nchi nyingi za EAC”Alisema Havugimana
Mwisho….