MKURUGENZI Mtendaji wa Benki ya Ushirika Tanzania (COOP BANK) Godfrey Ng’urah amebainisha asilimia za wawekezaji mkubwa wa kimkakati wa Benki hiyo kuwa ni pamoja na, vyama vya Ushirika ni asilimia 51,CRDB Benki asilimia 20,Taasisi na watu binafsi asilimia 19 na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni asilimia 10.
Mkurugenzi huyo ameyasema hayo mapema Leo hii Jijini Dodoma Januari 29,2025 katika mkutano wa Wahariri na Waandishi wa Habari kuelezea habari mpya ya sokoni ya Benki hiyo pamoja na Dira na Adhma ya 2025-2030.
Na kuongeza kuwa Umiliki jumuishi huo na wa kimkakati wa Benki utahakikisha uwepo wa mawanda mapana ya usimamizi na Utawala bora ili kuhakikisha uendelevu.
“Umiliki wa hisa na Utawala boraBenki ya Ushirika Tanzania (Coop Bank) kwa sasa inamilikiwa na wanaushirika kama wawekezaji wakuu na baadhi ya wawekezaji wa kimkakati kama ifuatavyo:Vyama vya Ushirika 51%Benki ya CRDB 20%Taasisi na watu binafsi 19%Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania-10%Umiliki huu jumuishi na wa kimkakati (Hybrid ownsrhip and Governace) ya Benki yetu, unatuhakikishia uwepo wa mawanda mapana ya usimamizi na utawala bora ili kuhakikisha uendelevu, uwazi na kubadilishana uzoefu kati ya falsafa ya kiushirika na dunia ya sekta binafsi na makampuni”.
Sambamba na hayo pia hakuacha kugusia kukua kwa kitabu, ambapo amesema Benki imekuza kitabu cha mikopo kutoka Shilingi milioni 320 mwaka 2020 hadi kufikia Shilingi bilioni 15 mwaka 2024 ikiwa ni sawa na ukuaji wa asilimia zaidi ya 5000 pamoja Benki kuimarisha ubora wa mikopo yake.
“Pia, benki imekuza kitabu chake cha mikopo toka shillingi milioni 320 mwaka 2020, hadi kufikia shillingi bilioni 15 mwaka 2024, sawa na ukuaji wa zaidi ya asilimia 5,000. Hata hivyo, Benki imeimarisha ubora wa mikopo yake, huku mikopo chechefu ikipungua toka asilimia (74%) ya mwaka 2020 hadi kufikia asilimia 2% kwa mwaka 2024Vilevile, amana za wateja zimeongezeka na kufikia bilioni 18 mwaka 2024 toka Bilioni 6 mwaka 2020, sawa na ukuaji wa asilimia 216% ndani ya miaka 4 ya mageuzi. Aidha jumla ya rasilimali za Benki zimekuwa na kufikia shilingi bilioni 50, mwaka 2024, toka shilingi bilioni 9.5, mwaka 2020, sawa na ukuaji wa asilimia 733%. Hii ni spidi ya Tai, au mwanga kama utapenda kuita hivyo. Na kwa hakika bado, tutawaonyesha watanzania, huduma za Benki zinawezekana kwa kila raia wa wa nchi hii na sio kwa watu wachache tu”.
Aidha ameongelea mafanikio mbalimbali waliyoyafanya kwa mwaka 2024 ikiwemo ukarabati na kuhamiq katika jengo lake jipya la makao makuu Dodoma toka Desemba 2024.
“Zaidi ya hayo, Benki imefanikisha haya yafuatayo kwa mwaka 2024:Ukarabati na kuhamia katika jengo lake jipya la makao makuu jijini Dodomatoka Decemba 2024,Kufungua tawi jipya Jijini Dodoma, pamoja na ujenzi na ukarabati wa matawi ya Tandahimba na Tabora Kuunganisha na kuboresha miundombinu ya Tehama na mifumo ya kutolea huduma za kibenki yaani (CBS) kutoka ya zamani kwenda mfumo mpya ya kidijitali (BR.Net) itakayochochea ukuaji wa huduma za kidigitali, ikiwa ni pamoja na huduma kwa njia ya simu na uwakala kupitia ofisi zote za vyama vya Ushirika kote nchini.Kwa mwaka huu wa fedha 2025, Benki itafungua matawi matatu ya kikanda Dar es salaam, Kagera na Mwanza”.
Akitoa salamu kwa niaba ya Serikali Dkt Benson Ndiege ambaye ni Mrajisi wa Vyama vya Ushirika amesema Ujio wa Benki hii unakuja kuchagiza maendeleo ya Ushirika katika kukuza Uchumi na maeneo mengine ya Kimkakati.
Aidha ameongeza kutoa wito na kuwapongeza wana ushiriki kwamba waendelee kutumia huduma za Benki lakini pia kuwapongeza kwa kusimama kidete katika kufanikisha maono haya tangu yalipoanz mwaka 2019 kwani wengi hawakuamini.
“Sasa nitoe wito kwa wana ushirika kwamba sasa Benki ipo na tuendelee kuitumia kwa huduma za Ki Benki”.
“Lakini wana ushirika nichukue nafasi hii kuwapongeza wanaushirika nchi nzima kwa kazi kubwa ambayo mmeifanya kwasababu maono haya mwanzoni mwa mwaka 2019 watu hawakuamini kwamba hili litatokea lakini wanaushirika walisimama kidete na Leo tumefika hapa, nawapongeza sana Wanaushirika na tuendelee kuchapa kazi”.
Uanzishwaji wa Benki hii ni miongoni mwa matokeo ya kimkakati ya Wizara ya Kikimo chini ya uongozi imara wa Mhe Waziri Mohamed Hussein Bashe aliyedhamilia kufanya mapinduzi ya kilimo kupitia sekta ya usharika kujiendesha kibiashara kupitia Benki mwamvuli wa wa kisekta itakayojibu changamoto za upatikanaji mitaji ya kilimo kwa wakulima.