MITAMBO YA SHILINGI BILIONI 1.7 YAZINDULIWA JIJINI ARUSHA

HAFLA ya uzinduzi wa malori mapya na mtambo mpya wa kutengeneza miundombinu ya barabara yenye thamani ya Sh.bilioni 1.7 imefanyika leo Jijini Arusha.

Akizungumza katika uzinduzi huo mgeni rasmi Meya wa Jiji la Arusha Macmillan Kirage amesema fedha ilitotumika kununua mitambo hiyo metokana na mapato ya ndani ya Jiji la Arusha na kusisitiza mitambo hiyo pia itahusika na ukarabati wa barabara zinazohusiana na Jiji, ambazo haziko chini ya usimamizi wa TARURA.

Aidha ametumia nafasi hiyo kuwasihi viongozi kuwahamasisha wananchi kupanda miti kwani kila halmashauri imepewa kama vile walivyopewa jukumu la kuhakikisha linapanda miti milioni moja na yote hayo ikiwa ni kuhakikisha Arusha inakuwa ya kijani.

“Hamasisheni wananchi kuhakikisha mnatunza mazingira .Pia wasitupe chupa za plastiki pembezoni mwa barabara kwenye daladala, mabasi ya abiria ili wazingatie usafi na Jiji like safi,”amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Arusha John Kayombo amesema mitambo hiyo imekuja ikiwa ni hatua muhimu ya kumaliza changamoto ya barabara mbovu katika maeneo mengi ya jiji hilo

“ununuzi wa mitambo hiyo ni matokeo ya juhudi za halmashauri kuhakikisha barabara za mitaa zinafanyiwa marekebisho kwa ufanisi, na kumaliza changamoto kubwa ya miundombinu ya barabara.”

Awali akisoma ripoti ya ununuzi wa mitambo hiyo Mhandisi wa Jiji la Arusha Jacobo Mwakyambiki amesema mitambo hiyo inathamani ya Sh.bilioni 1.7 na lengo ni kukarabati miundombinu ya Jiji la Arusha.


Related Posts