TBT yakutana na wadau wa chai kujadiliana uendelezaji wa zao

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Bodi ya Chai Tanzania (TBT) imekutana na wa wadau wa Chai katika kujadiliana na kuweka mikakati ya uendelezaji wa zao hilo.

TBT katiika uimarishaji wa zao la chai imeweka mikakati ya masoko ya Chai ambapo inahitaji uzalishaji wa chai ya kutosha kwenye masoko ya kimkakati yaliyowekwa.

Hayo yamebanishwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya chai Tanzania,Beatrice Banzi wakati wa kikao na wadau wa zao la chai kwa lengo kubwa lilikuwa kujadili namna ya kwenda kuongeza uzalishaji wenye ubora kutokana na chai inayozalishwa nchini ni bora.

Amesema changamoto zinazo likabili zao hilo umeme kukatika mara kwa mara pamoja na miundombinu ya barabara.

Banzi amesema kuwa katika kikao hicho kilicho wakutanisha wadau mbali ikiwemo Wizara ya kilimo,bodi ya chai yenyewe,Tantrade ,bandari ,watu wa ushirika ni kuweza kungumza kwa pamoja na kupanga mikakati jinsi gani wanaweza kufikia malengo yao waliojiwekea yakuendeleza zao la chai kwa muda wa miaka 10 kutoka 2024 mpaka 2034.

Amesema kuwa wanawezaje kufikia malengo hayo ni lazima watu wa Serikali ,watu wa sekta binafsi waweze kukaa chini kwa pamoja waweze kujadili ni jinsi gani wanaweza kuokoa zao hilo.

“Hapa ni kama tunafanya road map ili tuweze kujua tunaendaje endaje kama ni kuongeza uzalishaji wale wadau wanaohusika na uzalishaji tunapanga kwa pamoja tunafanyaje ,kama tuna taka kutangaza chai yetu ndani na nje ya nchi tunafanyaje kwashirikiana na tantrade kwa hiyo yale majadiliano yetu sisi washiriki wa mkutano wa leo ndiyo yatatumika kama road map yakuweza kuboresha huu mkakati ambao tumeupanga kwakuweza kuinua na kuendeleza zao la chai kwa miaka kumi ijayo”amesema Beatrice

Aidha amesema kuwa katika kikao hicho pia watatambulisha nembo ambayo wataitambulisha kwa wenzao wafanyabiashara ya chai ili iweze kutumika kuitambulisha chai inayozalishwa nchini ili hata ikiuzwa nje ya nchi mtu ajue chai hii inazalishwa Tanzania.

Hata hivyo Beatrice amesema kuwa bado kuna tofauti ya chai wanaokunywa watanzania na nje ya nchi hivyo wanaandaa mkakati wakuboresha chai inaonywea nchini na nje ya nchi iwe na viwango sawa vya ubora.
 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania (TBT) Beatrice Banzi akizungumza  na katika mkutano na wadau wa Chai (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.
 

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Chai Tanzania (TBT) Beatrice Banzi akizungumza  na waandishi habari kuhusiana na mikakati ya TBT katika uzalishaji  wa Chai nchini jijini Dar es Salaam.

 

Baadhi ya Matukio  katika picha kwenye mkutano wa wadau wa Chai ,jijini Dar e Salaam.

Related Posts