miche 1000 ya matunda ya Parachichi imetolewa bure kwa vijana Kupitia mradi wa BBT Njombe

Kupitia mradi wa BBT unaotarajia kuanza kwa vikundi vya vijana wilayani Njombe,miche 1000 ya matunda ya Parachichi imetolewa bure ili kuanza kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi kupitia zao hilo.

Akizungumza na Ayo TV shambani kwake mkulima maarufu wa zao hilo bwana Stiven Mlimbila alipotembelewa na baadhi viongozi wa mradi huo amesema yuko tayari kutoa mchango huo ili kuisaidia serikali kuwainua vijana wenzake kiuchumi.

“Nimewakabidhi miche hii 1000 nafikiri ni wao tu sasa kushughurikia kwa kuwa ni mwanzo mzuri kwa hawa vijana kwa kuwa ni fursa kwao na wamepata sehemu ya kuanzia”amesema Mlimbila

Mlimbila anasema biashara ya parachichi kwa Vijana BBT itawalipa kwa sababu yeye ana shamba la parachichi Ekari zisizozidi 50 ambazo amelima maparachichi na kwa msimu mmoja akivuna anaingiza Milioni 200

Mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amesema halmashauri ya mji wa Njombe imekwishatoa hekta tisini na tano ambapo hekta kumi zitakuwa kwa ajili ya kilimo hicho.

Vumilia Zikankuba ni mratibu wa programu ya BBT anasema kwa upande wao wako tayari kutoa fura ya mikopo kwa vijana ambao watakua tayari kuanza kilimo kwani tayari pesa zipo zinangoja vijana walio tayari kwaajili ya kukopa ili wajiendeleze.

Related Posts