BAADA ya kucheza mechi 11 bila ushindi wowote, Mlandizi Queens wiki hii itakuwa ugenini kujiuliza mbele ya JKT Queens.
Hadi sasa ndio timu iliyopo kwenye nafasi mbaya za kushuka daraja msimu huu ikipata sare moja huku kwenye mechi 11 nyingine ikigawa pointi tu.
Timu hizo zinakutana JKT ikiwa ya pili kwenye msimamo kwa pointi 26 huku Mlandizi ikisalia mkiani na alama moja pekee.
Mara ya mwisho zilipokutana timu hizo, JKT ilishinda 7-0 na kuwa timu ya kwanza kufungwa mabao mengi.
Akizungumza na Mwanaspoti, kocha wa timu hiyo, Jamila Rajabu alisema wanajua ugumu wa mchezo huo kutokana na timu wanayocheza nayo kuwa na ubora.
“Ni mchezo mgumu sana lakini tutakwenda kupambana hivyo hivyo hali yetu sio nzuri na tunatamani kufanya jambo angalau kutoka nafasi tuliyopo.”