USAID Ni Shirika La Kihalifu, Lifutwe – Global Publishers



Bilionea Elon Musk, ambaye anaongoza Kitengo cha Ufanisi wa Serikali ya Donald Trump nchini Marekani

Bilionea Elon Musk, ambaye anaongoza Kitengo cha Ufanisi wa Serikali ya Donald Trump nchini Marekani, amesema kuwa Shirika la Misaada la Marekani (USAID) ni shirika la kihalifu na kwamba watendaji wake wamekuwa wakilitumia kama kichaka cha kuiba fedha za serikali.

Trump amesema shirika hilo lipo kwenye hatua ambayo haiwezi kurekebishwa, na badala yake linatakiwa kufutwa, hatua ambayo amesema itasaidia kuokoa kiasi cha dola trilioni 1 kwa mwaka.

Kwa miaka mingi, Shirika la USAID limekuwa likitoa misaada kwa nchi maskini kwenye sekta mbalimbali, kuanzia afya za wanawake na watoto katika maeneo yenye machafuko, maji safi na salama, matibabu ya HIV/AIDS, sekta ya nishati, na maeneo mengine muhimu.

Tangu Trump atangaze kusitishwa kwa misaada inayotolewa na shirika hilo, dunia nzima imetikisika, na kauli ya Musk imetafsiriwa kama kutonesha kidonda ambacho hakijapona.

Bila kutoa ushahidi, Musk amelituhumu shirika hilo lenye wafanyakazi takriban 10,000 kuwa ni la kihalifu na kushauri lifutwe mara moja


Related Posts