Opah amfuata Singano Mexico | Mwanaspoti

NAHODHA wa timu ya Taifa ya wanawake ya Twiga Stars, Opah Clement amejiunga na FC Juarez ya Mexico anayochezea Mtanzania mwenzake, Julietha Singano.

Ukiachana na Simba Queens alikopata mafanikio makubwa ya soka la wanawake, nyota huyo alichezea Kayseri Kadın ya Uturuki kwa mkopo 2022, msimu uliofuata akasajiliwa Besiktas ya nchi hiyo na 2023/24 akiichezea Henan Jianye ya China kwa msimu mmoja.

Wote wawili waliichezea Simba Queens kabla ya kutimkia nchi nyingine, Julietha akitimkia Mexico na Opah akitambulishwa Uturuki.

Usajili huo unaifanya timu hiyo kuwa na nyota wawili Watanzania akiwamo Singano anayecheza beki wa kati kwa msimu wa tatu sasa tangu ajiunge nayo msimu 2022/23.

Hata hivyo, Opah anakuwa mchezaji wa kike wa tatu kusajiliwa nchi hiyo baada ya msimu uliopita Enekia Lunyamila kutambulishwa Mazaltan inayoshiriki Ligi hiyo.

Msimu uliopita akiwa na Henan, Opah alifunga mabao matano, Besiktas akifunga mabao sita na Kadin alipoweka kambani mabao matano.

Related Posts