Yao arejea Yanga baada ya dakika 360

BAADA ya kukosekana katika michezo minne iliyopita sawa na dakika 360, hatimaye beki wa kulia wa Yanga, Attohoula Yao amerejea uwanjani kwa kupangwa kuanza katika mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Simba ambao unachezwa leo, Jumamosi kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

Yao ambaye alipata majeraha katika mchezo wa ligi dhidi ya Azam, alikosa mechi mbili za robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelod Sundowns ya Afrika Kusini, Dodoma Jiji katika Kombe la Shirikisho (FA) na ligi dhidi ya Singida Big Stars.

Urejeo wake unamaana gani? Umemfanya kocha wa Yanga kumtua mzigo Dickson Job ambaye muda mwingine ilibidi kutumika eneo hilo kutokana na Kibwana Shomary kutokuwa fiti, ikumbukwe kuwa beki huyo naye matoka majeruhi.

Kurudi kwa Yao kunaongeza makali kwa Yanga katika upande wao wa kulia kutokana na beki huyo kuwa na uwezo mzuri wa kushambulia.

Yao ndiye kinara wa asisti kwa upande wa mabao, anaongoza akiwa na asisti saba huku kinara kwa wachezaji wote kiujumla akiwa na Kipre Juinio wa Azam aliyetoa asisti saba.

Related Posts