NIKWAMBIE MAMA: Kwenye haya, namwelewa Rais Trump

Paka ni kiumbe anayependa starehe na mambo mazuri. Hapendi vurugu wala shuruba hata kidogo. Paka anaweza kugoma kuondoka kwenye kochi anapokuona ukitaka kuketi hapo. Anaona kufanyiwa hivyo ni kuvurugiwa starehe yake ya kujilaza sofani, huku wewe ambaye ni bosi wake ukimpapasa kichwani. Kama vile yeye ndiye bosi wa nyumba, unapaswa kumletea ruzuku ya maziwa kila kunapokucha. Mkipika samaki au nyama mpelekeeni, ila maharagwe kuleni wenyewe.

Tukubali au tukatae, binadamu ana hulka zinazofanana na za paka. Duniani kote inajulikana kuwa inawapasa binadamu wafanye kazi ili waishi. Lakini hakuna nafsi inayopenda kushurutishwa. Sasa kwa vile kazi ni kitu cha lazima, watu wote wametokea kuichukia kazi. Wanaiona tofauti ya starehe na kazi kuwa sawa na ubwana na utwana.

Tangu enzi na enzi hakuna wakati unaotajwa kuwa mbaya zaidi ya wakati wa utumwa. Mtumwa hutimbika kwa faida isiyo yake, ila ya mtumaji. Daima mtumwa anaomba yeye abadilishwe kutoka mtwana kuwa bwana ili astarehe. Hapa tulipatwa na mzimu huo, tukapigana kujikwamua kuondokana na hali hiyo. Lakini baadaye tukadai kuachana na vifungo vyote, ikiwemo mikataba feki tuliyowekewa. Hivyo hakuna wakati unaopendwa zaidi duniani kama wakati wa ‘kula bata’.

Lakini kwa masikini ni zaidi. Kwa kuwa masikini hana uhakika wa kupata mahitaji yake, pindi anapokutana nayo anazidisha kipimo. Kwa mfano akipenyeza kwenye sherehe atajitahidi kumaliza sinia zima la pilau peke yake. Kama vinywaji ni vya kujihudumia ataokotwa hapo asubuhi akiwa hajitambui. Yote ni kwa sababu hana ujanja wa kujisosomola kwa uwezo wake, wala haijui nafasi nyingine kama hiyo itatokea wakati gani.

Waafrika tulivyotawaliwa, tulikoseshwa haki zetu zote za msingi. Nina maana ya elimu, imani, mahusiano, familia na kila kila kitu linachohusu utu wetu. Baada ya biashara hiyo kuuawa, tukaanza upya bila kujua pa kuanzia. Wengine walidhani aliyekomesha biashara ya utumwa alikuwa anawatetea waafrika, lakini historia inatupasha kuwa aliyeianzisha ndiye aliyeifunga na kuipiga vita.

Hali hii ndiyo iliyonifanya nimchukie Rais wa 57 wa Marekani, Donald Trump. Marekani ni taifa kubwa sana, kwani linawasaidia hadi mataifa yaliyo baba yake. Kama linaweza kujiingiza na kutoa maamuzi magumu huko duniani (kwa mfano Mashariki ya Kati), inamaanisha linaweza kuyaburuza mataifa saba duniani. Na tunaona jinsi Wamarekani wanavyoongoza misaada duniani kote iwe vitani, kwenye njaa, uzazi salama, magonjwa ya maambukizi na kadhalika.

Juzi kati Trump alitishia kukomesha misaada kwa Afrika. Kwa mtazamo wake anawaona watu hao wakizifisadi fedha za misaada kwa kuzilia bata kulekule walikosaidiwa. Anawafananisha na paka wa ndani wasiojua kutafuta, bali kupewa na kupetiwa. Kule mwanzoni Trump aliwahi kusema ingelikuwa jambo bora iwapo Afrika ingelitawaliwa kwa mara nyingine. Sasa anasema nia bora ya kumfundisha mtu umuhimu wa maji ni kukausha kisima chake.

Sasa amefikia kukatiza misaada ya kibinadamu inayotolewa na Marekani kwa Afrika. Haoni haja ya kuwasaidia watu wasiosaidika, mwisho wa siku waonekane kama mtu anayemsaidia mtwanga maji kwenye kinu. Inaeleweka ukifanya ishu zako na mwizi nawe utakuwa mwizi. Au kwa lugha nyepesi; mwizi wa simu akikamatwa kibarazani kwa mwizi wa benki, wa kwanza atapanda statasi lakini wa pili atashuka.

Kimsingi Trump yupo sawasawa. Wamarekani wamemwelewa kwa kipindi kingine, lakini wabongo tuna tofauti kubwa. Kwa sera zake, kama angekuja kupigiwa kura hapa bongo hangepata kura zaidi ya kura yake mwenyewe. Alikuwepo mzee wetu aliyekwenda kupigiwa kura na familia ya watoto kumi na wawili, majibu yalipotoka hakuambulia hata kura yake mwenyewe! Kisa ati sera yake ilikuwa ni kupiga vita rushwa.

Kiongozi yeyote anayenyosha maelezo hukosana na wengi. Hii ni kwa sababu Watanzania hawanyoshewi maelezo wakaelewa. Picha linaanzia pale ndoto za mwanafunzi zinavyokufa kwa sababu Serikali yake haijajiandaa kumuajiri. Fikiria mzazi anapoteleza na kumwambia mtoto wake “Kwanza wewe mi sikupanga kukuzaa”. Au “Sijui mamako kanipigapigaje. Tangu lini Msukuma nikatoa mbegu ya pimbi!”

Sasa basi mwanafunzi anayejiandaa kufanya mtihani wa darasa la saba, mtu aliyefeli ndiye aliyepelekwa Chuo cha Ualimu.

Ukweli anaousema Trump viongozi wa Kiafrika hawaupendi. Lakini mifano anayotoa ni michungu sana. Unahitaji akili ya kijinga kumpinga. Tunashindwa kumaliza matatizo yetu. Tuna rasilimali nyingi lakini tunategemea misaada ya wamarekan watujengee barabara.

Waafrika ameshatuambia kuwa sisi ni wavivu, zaidi tunaweza ngono na wizi, hiyo ni kweli. Hata mashoga kule kwao ameshawaambia watafute pa kwenda akiwa rais… Waarabu kawaambia wakatafute dunia nyingine ya kujitolea mhanga…

Viongozi wa Kiafrika kawaambia waache kuibia masikini hela na kwenda kuzificha Marekani, akiwa rais amesema atalala nao mbele…

Athari hizo zinatokana na Marekani kuwa mchangiaji mkubwa wa kifedha wa WHO na programu mbalimbali zilizopo chini ya shirika hilo na taasisi nyingine kubwa za kiafya duniani.

Katika kipindi cha miaka minne iliyopita, utawala wa Joe Biden uliziondolea nchi saba za Afrika stahiki zao katika mkataba wa AGOA kwa kutozingatia demokrasia.

Related Posts