Katika kuhakikisha wafanyabiashara wa soko kuu la kimataifa Kariakoo wanapata huduma zao karibu, Mkuu wa wilaya ya Ilala, Mkoani Dar es salaam Edward Mpogolo, amesema halmashauri hiyo ipo tayari kushirikiana na mamlaka nyingine ikiwepo TRA.
Mpogolo ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa Mkutano kati ya viongozi wa halmashauri, Kamishna Mkuu wa TRA YUSUPH MWENDA na jumuia ya wafanyabiashara Kariakoo.
Mpogolo amezungumza juu ya mikakati waliyojiwekea na wafanyabiashara wa Kariakoo wakiwepo machinga kufanya soko ilo kuwa rafiki na mazingira yenye kuleta faida kwa mlipa kodi.
Ameeleza nia njema ya wafanyabiashara endapo watakuwa katika mazingira rafiki ya kibiashara wanauwezo wa kulipa kodi, kuliko wanavyofanya sasa katika mazingira finyu ya barabarani.
Mpogolo ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwa kutowa fedha, kiasi cha shilingi bilioni 28 kwa ajili ya ujenzi wa soko jipya la kimataifa kariakoo, baada ya kuungua moto kwa soko la awali.
Huku shukrani nyingine kwa ajili ya Rais kutoa fedha za ujenzi wa soko jipya Jangwani, litalobeba wafanyabiashara wadogo, na kumtaka afisa biashara kuandaa kazi data ya wafanyabiashara waliopo kariakoo hivi sasa ili soko linapokamilika wapewe kipaombele na kuondoa malalamiko ya kukosa nafasi.
Mkuu huyo wa wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo amemuhakikishia kamishna Mkuu wa TRA YUSUPH MWENDA, ofisi yake iko tayari kutoa ushirikiano kwa jumuia ya wafanyabiashara kariakoo, pamoja na jumuia ya wafanyabiashara Dar es salaam, kwani serikali inatambua namna walivyoweza kutoa ajira kwa watu wengi na kulipa kodi.
Hali iliyomfanya Mpogolo kuwataka wafanyabiashara ambao hawamo katika umoja wajiunge ili waweze kusaidiwa kirahisi changamoto zao kupitia viongozi wao, na kunufaika na umoja kwa kutambuliwa rasmi.
Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa TRA YUSUPH MWENDA, amebainisha mchango mkubwa wa wafanyabiashara Kariakoo kwa kuzalisha walipa kodi wakubwa, wa kati na wadogojambo ambalo TRA inajivunia.
Kamishna huyo wa TRA amebaimisha mipango mitatu ya kuhakikisha umuhimu wa soko na wafanyabiashara Kariakoo moja wapo ni kuzalisha mabilionea wazawa na si kuzalisha mabilionea wageni kupitia soko hilo.
Nao wafanyabiashara wa soko la Kariakoo wamesema wako tayari kulipa kodi, ili wafanye biashara zao kwa amani wakati TRA imebainisha iko tayari kugharamia zoezi la kupata kazi data kwa wafanyabiashara wa Soko la Kariakoo waweze kutambulika rasmi.