Tanzania Yatengeneza Biosensor ya Kwanza Afrika Mashariki kwa Ulinzi wa Wanyama Pori

Na Karama Kenyunko, Michuzi Tv

IDARA ya Baolojia ya Molekyuli na baoteknolojia, kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) inahitaji taasisi au makampuni mbalimbali kutoka Tanzania na nje ya nchi ambayo wanaweza kushirikiana kutengeneza Chipu ya kihisio cha kibaolojia (Biosensor chips) itakayotumika kutambua au kujua uwepo wa virusi vinavyoshambulia wanyamapori kama simba, nyati na wanyama wengine katika mbuga za wanyama na kukusababisha mlipuko wa magonjwa.

Dkt. Ally Mahadhy, Mhadhiri na Mtafiti katika idara ya Baolojia ya Molekyuli na baoteknolojia, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) amesema haya hivi karibuni alipokuwa akiongea Michuzi Blog kuhusu baoteknolojia na jinsi inavyoweza kutumika kulinda wanyama pori katika mbuga za wanyama.

“Tunahitaji kushirikiana na taasisi za utafiti, usimamizi na uchunguzi kutoka Tanzania na nchi za nje kutengeneza biosensor chips kwa wingi zaidi ili zitumike kutambua virusi vinavyoshambulia wanyama pori na kusababisha magonjwa lakini pia kuimarisha sekta ya utalii,” anasema..

Amesema Lengo kuu ni kulinda wanyama pori ambao wanavutia watalii wengi kutoka nchi za nje kuja kutembelea Tanzania na wanaongiza fedha za kigeni, kuimarisha sekta ya utalii nchini na kusaidia serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi wake.

Hadi sasa idara imetengeneza kihisio cha kinasaba( ‘a DNA-based prototype biosensor device’ )inayoweza kutambua au kugundua kirusi kinachoitwa Canine Distemper Virus (CDV) ambacho kinashambulia sana simba, nyati na wanyama pori wengine katika mbuga za wanyama.

Hivi sasa kifaa hiki kinapatikana kwa taasisi ambazo zipo tayari kutengeneza Chipu ya kihisio cha kibaolojia (biosensor chips) kwa wingi zaidi ili kulinda wanyama pori na kuimarisha sekta ya utalii.

“Hii ndyo Biosensor ya kwanza kutengenezwa na wataalam watanzania kwenye ardhi ya Tanzania na Afrika Mashariki, ubunifu huu unatoa fursa ya kutengeneza biosensors nyingine kwa ajili ya kutambua magonjwa mbalimbali ya binadamu, wanyama na mimea,” anasema

Anasema magonjwa kwa binadamu kama HIV, Dengue na malaria, wanyama kama ‘Foot and mouth, Rabies na mimea kama Banana Wilt na Cassava Mosaic.

“Tumefanikiwa kutengeneza kifaa hiki kwa ufadhili wa Chuo kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) ambao walitoa shilingi milioni 30 ili tuweze kufanya utafiti kuhusu virusi vinavyoshambulia simba na wanyama pori wengine na kusababisha magonjwa kati yao,” anasema

Ameedelea kwa kusema kuwa taasisi zinazohitaji kushirikiana na sisi, hiki ni kifaa kinachotumia DNA kutambua virusi kwa wanyama pori.

Mbali na hilo, bado wanahitaji ufadhili wa kufanya sampo kwenye mbuga za wanyama ili kuona je kifaa hiki kinabehave vipi.ansema

Ameeleza, Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) inaweza kutumia kihisio cha kinasaba na Chipu ya kihisio cha kibaolojia kutambua virusi vinavyoshambulia wanyama pori katika mbuga za wanyama ambao wanasaidia Tanzania kupata fedha za kigeni.’

“Wameamua kutengeneza DNA-based biosensor device baada ya kugundua kuwa simba wanashambuliwa sana na kirusi kinachoitwa ‘Canine Distemper Virus (CDV) kuliko wanyama wengine. Mwaka 1994, asilimia 30 ya simba walikufa kutokana na kushambuliwa na kirusi cha CDV,” anasema

Sekta ya utalii inachangia asilimia 17.5 kwenye pato la Taifa na asilimia 25 ya fedha zote za kigeni.
 

Dkt. Ally Mahadhy, Mhadhiri na Mtafiti katika idara ya Baolojia ya Molekyuli na baoteknolojia, Chuo Kikuu cha  Dar es Salaam (UDSM) akionyesha namna ya kuunganisha Chipu ya kihisio cha kibaolojia (Biosensor chips) kwenye kompyuta kwa Mwandishi wa Michuzi, kifaa hicho kinatumika kutambua au kujua uwepo wa virusi vinavyoshambulia wanyamapori.
 

Dkt. Ally Mahadhy, Mhadhiri na Mtafiti katika idara ya Baolojia ya Molekyuli na baoteknolojia, Chuo Kikuu cha  Dar es Salaam (UDSM) akimuonyesha Mwandishi wa Michuzi, Chipu ya kihisio cha kibaolojia (Biosensor chips) inavyofanana, kifaa hicho kinatumika kutambua au kujua uwepo wa virusi vinavyoshambulia wanyamapori.

Related Posts