Rombo. Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango ameongoza mamia ya waombolezaji katika kanisa la Mtakatifu Pius wa X, Parokia ya Tarakea, wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro katika ibada ya Misa takatifu ya kumuaga mama mzazi wa Profesa Adolf Mkenda, mama Sekunda Massawe (82).
Mama wa Profesa Mkenda, ambaye alifariki dunia, Januari 30, mwaka huu atazikwa leo katika makaburi ya familia nyumbani kwake Kijiji cha Mbomai Juu, wilayani humo.
Viongozi mbalimbali wa Serikali na chama, wakiwamo mawaziri, wabunge wa Mkoa wa Kilimanjaro na wakuu wa wilaya za mkoa huo wanashiriki ibada hiyo ya Misa takatifu.
Ibada hiyo inaongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi, Askofu Ludovick Minde akiongozana na mapadre zaidi ya 40 wa Jimbo hilo.
Endelea kufuatilia Mwananchi digital kwa taarifa zaidi.