Hayo yameelezwa leo Jumatano tarehe 05 Februari 2024, na Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Lughano Kusiluka, alipokutana na kufanya mazungumzo na Bw. Edward Sundberg, Mratibu wa programu ya mafunzo kwa Afrika kutoka Shirika la “Africa Program for Cyber Technology (APCT)”.
Akizungumzia Programu hiyo, Bw. Edward amesema, mafunzo hayo yatatolewa kwa miezi sita kwa njia ya mtandao, kwa kuanza na kundi la wanafunzi 200, kwa usimamizi wa wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma, Ndaki ya Sayansi za Komputa na Elimu Ngavu kwa ushirikiano na Washirika wa programu hiyo waliopo nchini Marekani. Aidha, kabla ya kupaya cheti, wanafunzi wote watafanya mitihani ambayo itaandaliwa kwa lengo la kuthibitisha ubora.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Prof. Lughano Kusiluka, akiwa kwenye mzungumzo ofisini kwake Dodoma na Bw. Edward Sundberg, Mratibu wa programu ya mafunzo kwa Afrika, kutoka Shirika la “Africa Program for Cyber Technology (APCT)”.
Bw. Edward Sundberg akiwa ameketi na Dkt. Florence Rashid, Kaimu RASI wa Ndaki ya Sayansi za Komputa na Elimu Ngavu, wakati wa kujadili kuhusu programu ya mafunzo ya Uthibitisho wa Wataalam wa Usalama Mtandaoni (Cybersecurity Professional Certification Program).
Prof. Lughano Kusiluka, akimsikiliza kwa makini Bw. Edward Sundberg, alipotembelea Makao Makuu ya UDOM, Dodoma.
Bw. Edward Sundberg (Katikati), akikabidhiwa zawadi na Prof. Lughano Kusiluka(Kulia kwa Bw. Edward), akiwa ameambatana na wasaidizi wake, Prof. Razack Lokina, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma (wa kwanza kushoto), na Prof. Winester Anderson (wa kwanza Kulia). Anayefuata kutoka kulia ni Dkt. Florence Rashid, Kaimu RASI wa Ndaki ya Sayansi za Komputa na Elimu Ngavu.
Prof. Kusiluka akiagana na Bw. Edward Sundberg, ofisini kwake Dodoma.