Wateja wa Benki ya FBME wasotea amana zao miaka saba, waiangukia Serikali

Dar es Salaam. Waliokuwa wateja wa Benki ya FBME zaidi ya 6,000 wameiangukia Serikali wakitaka kuharakishwa kwa mchakato wa malipo ya amana zao zinazodaiwa kuwa zaidi ya Sh31 bilioni wanazodai kwa takribani miaka 7 sasa.

Benki hiyo iliwekwa chini ya ufilisi Mei mwaka 2017 baada ya Marekani kuituhumu FBME tawi la Tanzania kuhusika na utakatishaji fedha jambo ambalo lilifanya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuiweka chini ya uangalizi.

Akizungumza na wanahabari kwa niaba ya wadai wengine, Dk Majura Mfungo amesema tangu benki hiyo ifungwe mwaka 2017, malipo ya amana za wateja na wadai wengine zaidi ya Sh31 bilioni bado hazijalipwa huku wengine wamefariki dunia.

“Pia, kumekuwa na kesi kadhaa ambazo zilipelekea malipo ya amana za wateja kuchelewa kulipwa, lakini hata baada ya kesi hizo zote kumalizika pamekuwa na usiri na sintofahamu ya ulipaji wa fedha za wateja,” amesema Dk Mfungo.

Akizungumzia suala hilo, Meneja Uendeshaji wa Bodi ya Bima ya Amana (DIB), Nkanwa Magina amesema zipo hatua ambazo zimechukuliwa kwa ajili ya kulipa amana hizo.

“Kuna kamati iliundwa kupitia taarifa za madeni hayo na kama kuna malalamiko yoyote wapelekewe na sisi tunayachukua kwao na kufanyia kazi na huu mkutano uliofanyika hatukua tunafahamu,” amesema.

Pia, aliwataka wateja hao kuendelea kujaza nyaraka mbalimbali zinazotakiwa ili waweze kulipwa amana zao kwa kile alichobainisha kuwa ambao walijaza baadhi wameshalipwa.

“Tunawalipa hela, tangu mwaka jana tuneshalipa asilimia 30, sasa kwa sababu benki ilikiwa chini ya ufilisi tunaendelea kuwalipa na huwa tunakutana na kamati ya madai mara kwa mara,” amesema.

 Alipokuwa akizungumza na wanahabari juu ya hatua ambazo zimewahi kuchukuliwa, Dk Mfungo amesema Desemba 29, 2023, DIB walitoa tangazo likiwataka wateja na wadai wengine kupeleka nyaraka muhimu ili malipo yao yaweze kufanyiwa kazi.

Baadaye waliongeza tena miezi miwili toka Januari Mosi 2024 hadi Februari 29 jambo ambalo lilifanya wapate matumaini ya fedha hizo kutoka.

 “Lakini Baada ya vikao kadhaa DIB walianza kulipa waliokuwa wateja wa benki Aprili na Mei 2024 na kiasi cha Sh8.67 bilioni ndiyo kililipwa kama asilimia 30 kwa wateja wote kwa ahadi kuwa kiasi kingine cha kukamilisha malipo yaani asilimia 70  kingelipwa ndani ya miezi sita toka siku ya kuanza malipo hayo kwa mujibu wa kanuni na taratibu zao za ufilisi,” amesema.

Amesema jambo hilo linatajwa kuwa kinyume na mwongozo wao wa ufilisi unaotambua malipo yanatakiwa yawe ndani ya siku 90.

“Hata hivyo sasa ni zaidi ya miezi tisa hakuna malipo yoyote yaliyofanyika kwa utimilifu hata viongozi wetu wanapofuatilia wamekuwa wakikosa majibu mazuri na kukosa matumaini ya kupata fedha zetu,” amesema.

Amesema jambo hilo linawavunja moyo kwani awalu walikuwa wakijibana na kuweka akiba ili ziwasaidie, lakini juhudi zao zimefia kwenye mikono ya DIB.

Dk Mfungo amesema jambo hilo linawapa ukakasi kama fedha hizi zipo au zimeshaliwa.

“Hiyo ni kwa kile walichokieleza kuwa katika kikao ambacho DIB ilikaa pamoja na kamati ya wateja iliwaeleza kuwa kuna fedha zinangojewa kutoka Cyprus na pindi zitakapotolewa fedha hizo Tanzania itakuwa miongoni mwa wanufaika.

“Lakini hadi sasa kamati ya wadai haijui fedha toka Cyprus zimeletwa tayari au bado kutokana na usiri uliopo.

“Hata kamati iliyochaguliwa kuwakilisha wateja wote wa FBME inayoongozwa na Mwenyekiti Mzee Mbakileki imeshindwa kuhakiki wateja wa Cyprus wakati huku ndiko makao makuu, je kuna wateja hewa au kuna nini kiko nyuma ya pazia kwa nini kamati isiruhusiwe kuhakiki majina ya wateja wa Cyprus kama ilivyofanya kwa majina ya wateja wa Tanzania,” amesema.

Septemba 2023, DIB ilisema kuna Sh2.9 bilioni za waliokuwa wateja wa benki mbalimbali zilizofungwa hazijachukuliwa, licha ya kutoa taarifa mara kwa mara.

Hata hivyo, kiasi hicho ni kile kilichopo kwenye kinga ya amana ambapo mpaka Februari mwaka huu ilikuwa ni kwa amana zisizozidi Sh1.5 milioni.

DIB wanasema tangu mwaka 2000 hadi Juni mwaka huu, jumla ya benki tisa ziliwekwa kwenye mufilisi, lakini ni asilimia 75 pekee ya wenye amana wamechukua amana zao.

Benki hizo tisa ni Greenland Bank

Tanzania Limited (2000), Delphis Bank Tanzania Limited (2003), FBME Bank Limited (2017), Mbinga Community Bank Plc (2017), Njombe Community Bank Limited (2018) na

Nyingine ni Bank Limited (2018), Covenant Bank for Women (T)

Limited (2018), Kagera Farmers’ Cooperative Bank Limited (2018) na Efatha Bank Limited (2018).

Related Posts