Na Humphrey Shao, Michuzi Tv
Wito umetolewa kwa wakandarasi kukamilisha kazi kwa wakati hili kutoa taswira ya hali ya fedha zinazotolewa na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa wanachi wake.
Wito huo umetolewa leo na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar-es-Salaam Omary Kumbilamoto akiwa katika ziara yake ya kutembelea miradi iliyokuwa imekwama na sasa imekwamuliwa na kupewa wakandarasi wengine, ambapo leo ametembelea Kata ya Majohe Mtaa Viwege kukagua Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya chenye Thamani ya Tsh. million 500.
” pesa hizi zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na sisi Halmashauri tumepewa dhamana ya kuwa wasimamizi hivyo atuwezi kukubali sisi tuonekane kikwazo cha kuwa ndio tunamkwamisha Rais wakati nyie mmepewa kila kitu ambacho kinawezesha mradi huu kukamilika” amesema Kubilamoto.
Kumbilamoto amesema kuwa ifike mwisho wa wakandarasi au mafundi waliopewa kazi kufanya kazi kwa mazoea na kupelekea hasara kwa serikali kwani sisi kama halmashauri tumejifunza na atutacheka na mzembe yoyote aliyepanga kuja kutukwamisha.
katika ziara hiyo mstahiki meya Kumbilamoto alipata kuongozana na Diwani wa Kata ya Majohe Pascal Linyamala na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Majohe Nuru Mizumo na Katibu wa CCM Kata ya Majohe Ndg. Pius Kagete wote kwa pamoja walitoa Shukrani kwa Mstahiki Meya kwa kufanya ziara ya kukagua ujenzi wa kituo hicho, ambacho kilisimama kwa muda mrefu bila Muendelezo na huku wananchi wakiendelea kuteseka na kumuomba awafikishie salamu za shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan.