Majeruhi wanne ajali iliyoua Saba morogoro waruhusiwa kutoka hospitali

Majeruhi wanne kati ya watano waliokuwa wanatibiwa katika hospitali ya Wilaya Mvomero waliotokana na ajali iliyoua watu saba wameruhusiwa kutoka hospitali huku mmoja akipelekwa hospitali ya Rufaa Mkoa Morogoro kwa matibabu zaidi.

Akizungumza na ayo tvna Millard ayo .com Mganga mfawidhi hospitali ya Wilaya Mvomero Dokta Frances Paul amesema majeruhi hao wanne walitibiwa na kuruhusiwa huku mmoja hali yake ikabadilika na kulazimika kupewa Rufaa na kuwa na idadi ya majeruhi wawili kutoka hospitali hiyo kupelekwa hospitali ya Rufaa baada ya Mmoja kupelekwa jana muda mchache baada ya kutokea ajali.

Ikumbukwe kuwa mei 14 mwaka huu eneo la dakawa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro barabara kuu ya Morogoro -Dodoma ilitokea ajali iliyohusisha gari aina ya Toyota Noah iliyokuwa na watu 13 kugongana uso kwa uso na na Lori la mzigo na kusababisha Vifo vya watu saba na majeruhi sita ambapo hadi Sasa wanne wameruhusiwa na wawili wanapatiwa matibabu hospitali ya Rufaa mkoa Morogoro.

Related Posts