Leo tumeshiriki katika hafla ya uwekaji saini mikataba ya kusimamia mikopo 10% ya fedha za Halmashauri iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma.
Benki ya CRDB imeshinda tenda ya kusimamia mikopo hiyo kutoka katika Halmashauri 5 kwa awamu ya kwanza kwa ajili ya wanawake, vijana na makundi maalum. Benki ya CRDB tunajivunia kuwa sehemu ya mpango huu muhimu unaolenga kukuza uchumi wa makundi mbalimbali na jamii kwa ujumla.
Katika utekelezaji wa mpango huu tutashirikiana na taasisi yetu ya @crdbbankfoundation ambayo imejikita katika ujumuishi wa kifedha na uwezeshaji wa wanawake na vijana katika jamii.
Mgeni Rasmi katika hafla hiyo alikuwa ni Waziri wa Nchi Ofisi Rais – TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa aliyeambatana na uongozi wa Wizara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule akiwa ndio mwenyeji wetu.
Benki ya CRDB iliwakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, @Tully_esther_mwambapa aliyeambatana na viongozi kutoka makao makuu na kanda ya kati ya Benki yetu.