NA Mwandiahi wetu
KATIBU wa siasa na uenezi na Mafunzo chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Bagamoyo,Ramadhani Lukanga anatarajia kuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa soko binafsi kitongoji cha kwakibosha kata ya Mapinga wialya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Uzinduzi wa soko binafsi ndani ya kitongoji kwa kwakibosha umekuja kufiatilia kilio cha miaka mingi cha wananchi wa kitongoji kukosa kosa la karibu.
Akizungumza wakati wa utoaji wa taarifa hiyo Mwenyekiti wa kitongoji cha kwakibosha Shabani Rashidi Athumani alisema ninadira ya maendeleo ya miaka mitano na moja shabaha katika dira hiyo ni soko.
“Eneo la soko binafsi lilipatikana mwezi wa 12 mwaka jana na vijana wanaosimamia tunashirian nao vema ndani ya ofisi ya kitongoji wameonyesha uwezo wao wa kiutendaji huku wakinitaji mimi kuwa kama mlezi wao na hatimae jumamaosi ndio wanazindua “alisema shabani na kuongeza…
” Napenda vijana wanaojituma pindi wanapoona fursa sikutegemea waliponiambia kuwa soko hilo binafsi linauwezo wa kuhudumia watu 200 kwa kuwapangia vizimba”
“Tunashukuru tumempata mwenyekiti wa kitongoji kijana ambae ni mzaliwa wa kibosha ameweza kuona changamoto tunazopata sisi wazazi wake kwani tumeshoka kila siku kwenda kuwapelekea wezetu utajiri’alisema Lucy Nkya na kuongeza….
Wamepeta viongozi watatu katika hiki kitongozi suala la soko wanaliongelea tu kwenye mikutano na makaratasi na kwa soko hili naamini historia itaandikwa kiongozi kijana huyo sasa kazi iendelee.
Hata hivyo mwenyekiti shabani amesema anawakaribisha wanamapinga wote kuja kujionea ubunifu pamoja na kujifunza mambo mbalimbali yatakayojili siku hiyo ya uzinduI wa soko hilo binafsi.