Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema sekta ya utalii ina mchango mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa nchi kupitia usafiri wa anga ambao ni kichochea kikuu cha ukuaji wa uchumi.
Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipofungua Kongamano la sita la usafiri wa anga Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Hoteli ya Verde Mtoni, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 15 Mei 2024.
Aidha Rais Dk.Mwinyi ameeleza hatua iliyofikiwa na SMZ katika ukuaji wa sekta ya usafiri wa anga ya kutekeleza miradi kwa kukamilisha jengo la abiria uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume Terminal 3, kuanza ujenzi jengo jipya la abiria Terminal 2 litakalohudumia abiria zaidi 1,300,000 kwa mwaka, ujenzi na ukarabati wa ujenzi wa jengo la zamani la Terminal 1.
Kadhalika ameongeza pia ujenzi wa jengo la biashara na ofisi katika jengo la tatu la abiria, jengo la kuhifadhi na kusafirisha hasa chakula vinavyoharibika kwa haraka, ujenzi wa vituo vitatu vya huduma za mafuta ya ndege, ujenzi wa uwanja wa ndege na upanuzi wa kiwanja cha ndege Pemba na jengo jipya la abiria na uwanja wa ujenzi wa kiwanja cha Nungwi.
Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amewahimiza washiriki wote wa kongamano hilo kujadili na kutoa mapendekezo kwa kubainisha fursa zitazoweza kutumika katika sekta ya usafiri wa anga kwa manufaa ya Nchi wanachama wa Jumuiya ya Mashariki.
Wakati wa salamu, Mwenyekiti wa Bodi ya Shirikisho la Usalama wa Anga Kanda ya Afrika Mashariki ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari amebainisha malengo makuu ya mkutano huu kuwa ni Kudumisha Mifumo Imara, Endelevu, Ubunifu, Usalama wa Usafiri wa Anga.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kulifungua Kongamano la 6 la Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, linalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar .
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirikisho la Usalama wa Anga Kanda ya Afrika Mashariki ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Sita la Afrika Mashariki la wadau wa masuala ya Usafiri wa Anga linalofanyika visiwani Zanzibar.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ally Mwinyi akiteta jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirikisho la Usalama wa Anga Kanda ya Afrika Mashariki ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bw. Hamza Johari wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Sita la Afrika Mashariki la wadau wa masuala ya Usafiri wa Anga linalofanyika visiwani Zanzibar.
Meza kuu ikifuatilia ufunguzi wa Kongamano la 6 la Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, linalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar.
Wadau wakiendelea kufuatilia ufunguzi wa Kongamano la 6 la Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, linalofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Verde Mtoni Zanzibar Wilaya ya Mjini Unguja Jijini Zanzibar leo.