Namibia. Baba wa Taifa la Namibia, Sam Nujoma amefariki dunia jana Jumamosi Februari 8, 2025 akiwa anapatiwa matibabu nchini humo.
Taarifa za kifo chake zimetangazwa leo Jumapili, Februari 9, 2025 na Rais wa sasa wa Namibia, Nangolo Mbumba.
Sam Nujoma, atakumbukwa kwa kuiongoza Namibia kupata uhuru mwaka 1990 na kuhudumu kama Rais wake wa kwanza kuanzia 1990 hadi 2005.
“Baba yetu mwanzilishi wa Taifa, aliishi maisha marefu na yenye matokeo ambayo alitumikia kwa njia ya kipekee watu wa nchi yake anayoipenda. Baba yetu Mwanzilishi aliwapanga kishujaa watu wa Namibia wakati wa saa za giza za mapambano yetu ya ukombozi hadi kupatikana kwa uhuru na uhuru Machi 21, 1990.
“Akiwa Rais mwanzilishi, Dk Sam Nujoma alijitoa kiuongozi kwa hali ya juu kwa taifa letu na hakuacha jitihada zozote za kuhamasisha kila Mwanamibia kujenga nchi ambayo ingesimama kidete na kujivunia miongoni mwa mataifa ya dunia,”ameandika Rais Mbumba
Nujoma amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95.