-Ni utekelezaji wa Mwaselela Ahadi umepeta
NA TATA GORDON KALULUNGA
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Ndele Jailos Mwaselela, ameendelea kutekeleza Ahadi zake kwa chama hicho ambapo Mwezi huu Februari 2025 amesema atakamilisha katika Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Amesema leo (jana) Februari 8,2025 atakabidhi bati Kata ya Isangala kama walivyoomba, kisha kuendelea na Kata zingine.
Mara tu baada ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo Februari 14,2023 alifanya ziara katika Wilaya zote na kutekeleza Ahadi katika Wilaya ya Kyela, Rungwe, Chunya na Mbeya Vijijini.
Katika Wilaya ya Kyela alitoa Mbao za kutosha jengo Zima kuezeka ofisi ya Wilaya hiyo, Rungwe alikarabati ofisi, Chunya alitoa Tofali ngazi ya Wilaya na Mbeya Vijijini pia alitoa Tofali kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Wilaya ambako pia alipokea maombi ya ukarabati wa ofisi za Kata za Chama hicho.
Katika maombi hayo, amesema atakamilisha Ahadi yake ya kukarabati ofisi za Chama hicho ndani ya Mwezi huu kutokana na uhitaji wa kila Kata.
Mbeya Vijijini ina Kata za Serikali 28 huku chama Cha Mapinduzi (CCM) kikiwa na Kata 32.