AA YANG’ARA KWENYE MASHINDANO YA CYBER CHAMPIONS YA MWAKA 2025.

 


Chuo cha Uhasibu Arusha kimeibuka kidedea na kung’ara katika mashindano ya Cyber Champions ya mwaka 2025

Mashindano hayo yameweza kushirikisha Taasisi za Elimu ya juu zaidi ya 40 na yamefanyika jijini Dodoma yakilenga kuibua vipaji, kuimarisha uelewa wa usalama mtandaoni na kuwaandaa vijana kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kidijiti.
Mashindano hayo adhimu ya kusaka vijapaji kwa vijana katika nyanja ya Tehama yameandaliwa na kuratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Bendera ya Chuo cha IAA imepeperushwa vyema na mwanafunzi John Mange, ambaye ameshika nafasi ya pili kati ya wanafunzi 600 waliyo shiriki katika mashindano hayo na pia kushika nafasi saba za juu kati ya nafasi 10 za juu za ushindi.
Aidha Chuo cha IAA kimefanikiwa kutoa washindi saba (07) katika washindi kumi (10) bora (Top Ten) wa mashindano hayo na kuzidi kuonyesha uimara wake wa kufua vijana katika nyanja ya kimtandao ambapo kwasasa ndipo dunia inaelekea na kuweza kupunguza wimbi la ajira nchini na kuzalisha wataalam bora wenye uwezo wa kitaifa na kimataifa.
Mkuu wa Chuo hicho Prof. Eliamani Sedoyeka Amesema lengo kuu la chuo ni kutoa wataalam wenye uwezo na watao kubalika sokoni na watakaotumia elimu na ujuzi wao kutatua changamoto katika jamii ndani ya nchi na nje ya nchi.
“Kwa sasa Chuo tumewekeza katika miundombinu ya TEHAMA, mitaala na rasilimaliwatu, IAA kupitia Mradi tuliyo nao wa HEET tunajenga kituo kikubwa cha umahiri cha TEHAMA, ambapo mtu yeyote atakayehitaji suluhisho la changamoto yoyote ya TEHAMA atakuja IAA na kupata ufumbuzi”.amesema Prof, Sedoyeka

Related Posts