Netanyahu awa mbogo mahakamani, tuhuma za rushwa zamtafuna

Mwanza. Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amepanda kwa mara nyingine kizimbani katika mahakama mjini Tel Aviv nchini humo kujibu mashtaka ya muda mrefu ya rushwa yanayomkabili.

Mashtaka yanayomkabili Netanyahu, ni mwendelezo wa majanga dhidi ya waziri mkuu huyo ambaye hivi karibuni, majaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), walitoa hati maalumu ya kukamatwa kwa Netanyahu kwa kutekeleza makosa ya uhalifu wa kivita.

Netanyahu (75) aliwasili mahakamani jana Jumatatu Februari 10, 2025, akiwa na mawakili wake, wakiongozwa na, Amit Hadad, baada ya kuamriwa kutoa ushahidi katika kesi tatu za rushwa za mwaka 2019, zinazohusisha kupokea zawadi kutoka kwa marafiki mamilionea.

Miongoni mwa mamilionea wanaotajwa kumpa hongo Netanyahu ni, Shaul Elovitch ambaye ni mshika dau kwenye Kampuni ya mawasiliano ya Bezeq.

Pia, anashtakiwa kwa madai ya kufanya makubaliano ya kisheria na wamiliki wa vyombo vya habari ili waripoti habari chanya kumhusu (Netanyahu) sambamba na kukubali zawadi za gharama kubwa kwa maslahi binafsi.

Hata hivyo, Waziri Mkuu, Netanyahu amekana mashtaka yote yanayomkabili. Netanyahu ni waziri mkuu wa kwanza wa Israel kushtakiwa kwa uhalifu.

Elovitch anadaiwa kupanga usambazaji wa taarifa chanya kuhusu Netanyahu na familia yake katika tovuti ya Walla.

Wakati wa kusikilizwa kesi hiyo, Jaji Rebecca Friedman-Feldman alimtaka wakili wa Netanyahu, Amit Hadad, kupunguza muda anaotumia kufafanua mifano zaidi ya 300 iliyo katika hati ya mashtaka kuhusu madai ya kuingilia uhuru wa vyombo vya habari yanayomkabili Netanyahu na wenzake.

 Hadad alikataa ombi hilo, akisema waendesha mashtaka wanapaswa kuondoa mifano isiyoonekana kuwa muhimu kabla ya kukubaliana na ombi la mahakama.

Baada ya hoja hiyo, Jaji huyo akatishia kuahirisha shauri hilo hadi wiki ijayo kwa ajili ya kuendelea na usikilizwaji wake jambo ambalo lilimfanya Netanyahu kulipuka mahakamani kisha shauri kuendelea kusikilizwa.

Uamuzi wa Jaji, Friedman-Feldman kuahirisha shauri hilo ulimfanya Netanyahu alipuke kwa hasira dhidi ya waendesha mashtaka baadaye katika kesi hiyo huku akisema “hamuoni aibu.”

Hati ya mashtaka ilieleza kuhusu makala iliyochapishwa kwenye tovuti ya Walla, Desemba 2014, ilielezea namna mtoto wa Netanyahu, Avner, alivyojiunga na Jeshi la Israel (IDF).

Waendesha Mashtaka wa Serikali,  wanadai kuwa Netanyahu alihusika katika kudai habari hiyo ichapishwe kama sehemu ya makubaliano yanayodaiwa kuwepo kati yake na Elovitch ili kuthibitisha uwepo wa mtoto wake jeshini.

Hadad alionyesha vyombo vingine vingi vya habari, kama NRG, Ynet, na Haaretz, vinavyoongoza kwa kumkosoa, Netanyahu, navyo vilichapisha habari hiyo, akisisitiza kuwa kulikuwa na msukumo wa kifedha wa tukio hilo kuripotiwa.

“Inakuwaje nashitakiwa kwa hili wakati limechapishwa kila mahali, hata na rafiki yangu (mchapishaji wa Haaretz Amos) Shocken,” Netanyahu alihoji kwa hasira.

“Kwa miaka minane, mmekuwa mkinivuta katika jahanamu hii. Kwa nini? Hamna aibu?,” alihoji Netanyahu.

“Hili ni jambo la kushangaza… Je, mlilichunguza hili?…Hamkukagua chochote. Mnawezaje kusema kwamba hili ni ‘upendeleo maalum?’ Mmenitegea mtego kutoka mwanzo hadi mwisho!” alisisitiza kiongozi huyo.

Awali, Hadad aliionyesha mahakama, mfano mwingine kwenye hati ya mashtaka unaodai Netanyahu aliingilia uhuru wa vyombo vya habari, kwa kumtaka, Elovitch na Mkurugenzi Mtendaji wa Walla, Ilan Yeshua, kuchapisha upya makala inayoeleza matumizi mabaya ya fedha yaliyofanywa na mke wa Waziri mkuu huyo, Sara Netanyahu.

Kutokana na maelezo hayo ya Hadad, Netanyahu aliwashutumu waendesha mashtaka kwa kujumuisha mfano huo katika hati ya mashtaka, akisema kuwa ni jambo la kawaida kabisa kudai kuomba makala ijumuishe mambo ya msingi kwenye habari yoyote.

Pia, akikiri kuhusika katika kutayarisha maudhui ya makala hiyo kwa kile alichodai ilikuwa ikimhusu moja kwa moja Mje wake (Sara) huku akidokeza kuwa msemaji wake, Nir Hefetz, ndiye aliyewasilisha mapendekezo yake kwenye ofisi za Wall

Related Posts