Saudia Yapewa Idhini Kuendesha Bandari Ya Bagamoyo – Global Publishers



Serikali ya Tanzania imeipa Kampuni ya Uwekezaji na Maendeleo ya Saudi-Afrika (SADC) haki ya uendeshaji na usimamizi wa Bandari ya Bagamoyo.

Taarifa zilizotolewa na Shirika la Habari la Saudi (SPA), likimnukuu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyabiashara wa Saudi, Hassan Al-Huwaizi imesema Idhini hiyo ni sehemu ya mradi wa “East Gateway” wa SADC, unaolenga kukuza biashara na uwekezaji katika eneo la Afrika Mashariki.

Hatua hiyo itaongeza nafasi ya Saudi Arabia kama mhimili mkuu wa maendeleo ya uchumi wa dunia, kuvutia uwekezaji mkubwa wa kigeni (hasa barani Afrika), na kuimarisha uwezo wake wa kimkakati katika usafirishaji wa bidhaa zake kwenda kwenye masoko ya kimataifa.

Katika Kongamano la Kibiashara kati ya Saudi Arabia na Tanzania, lililofanyika kwa msaada wa Vyama vya Wafanyabiashara wa Saudi, Ufalme huo umechukua hatua ya kimkakati kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na Zanzibar pamoja na kutafuta fursa mpya za uwekezaji katika ukanda huu.

Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati mpana wa Saudi Arabia wa kupanua uwepo wake katika masoko ya Afrika.

Bandari ya Bagamoyo inashikilia thamani kubwa ya kimkakati kwa Saudi Arabia, kwani inatarajiwa kuwa lango kuu la biashara kwa Afrika Mashariki.

Bandari hii itarahisisha biashara kwa Tanzania na nchi jirani, na kuwa kitovu cha usafirishaji wa malighafi na rasilimali za asili kutoka Afrika kwenda duniani, sambamba na kuingiza bidhaa kutoka nje kuja barani Afrika.


Related Posts