Serikali yawaita kazini watumishi wapya 600, majina haya hapa

Dar es Salaam. Serikali imewaita watumishi zaidi ya 600 wa kada mbalimbali kuripoti kazini katika muda ambao utakuwa umepangwa katika barua za ajira watakazopewa.

Majibu yaliyotolewa ni ya wale ambao waliofanya usaili kati ya Septemba 2, 2024 na Januari 17, 2024 na kufaulu ambayo yameunganishwa na mengine kutoka kanzidata.

Taarifa kwa umma iliyotolewa na Sekretarieti Ya Ajira Katika Utumishi Wa Umma na kusainiwa na Katibu wa Sekretarieti ya Ajira inaeleza kuwa orodha ya majina haya pia inajumuisha baadhi ya wasailiwa waliokuwa kwenye kanzidata (Database) kwa kada mbalimbali.

Majina ya waliokuwapo katika kanzidata yamechukuliwa na kupangiwa vituo vya kazi baada ya nafasi kupatikana.

>>Majina ya watumishi wapya haya hapa

Taarifa inasema kuwa waombaji waliofaulu usaili wanatakiwa kuchukua barua za kupangiwa kituo cha kazi katika Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma zilizopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kwenye Majengo ya Dk Asha Rose Migiro, Masjala ya wazi ndani ya siku saba kutoka tarehe ya tangazo hili.

“Baada ya hapo barua ambazo hazitachukuliwa na wahusika zitatumwa kupitia anuani zao za Posta,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Pia, waombaji kazi waliofaulu usaili na kupangiwa kituo cha kazi wametakiwa kuripoti kwa mwajiri katika muda ambao umeainishwa kwenye barua za kupangiwa kituo cha kazi wakiwa na vyeti halisi vya masomo kuanzia kidato cha nne na kuendelea ili vihakikiwe na mwajiri kabla ya kupewa barua ya ajira.

“Kwa wale ambao majina yao hayapo katika tangazo hili watambue kuwa hawakupata nafasi/hawakufaulu usaili, hivyo wasisite kuomba kwa mara nyingine nafasi za kazi zitakapotangazwa,” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.

>>Majina ya watumishi wapya haya hapa

Uchambuzi unaonyesha kuwa waajiriwa hawa wameelekezwa katika mikoa ya Singida, Tanga, Mara, Mbeya, Tanga, Njombe, Mwanza na Arusha.

Mbali na ualimu nafasi nyingine ambazo watu wamepangiwa ni afisa ugavi daraja la II, Msaidizi Wa Mifugo Daraja La II, Fundi Sanifu Maabara Ya Shule Daraja La II, Afisa Usafirishaji Daraja La II, Afisa Maendeleo Ya Jamii Msaidizi Daraja La II, Mkadiriaji Majenzi Daraja La II.

Nafasi Nyingine Ni Fundi Sanifu Daraja La II, Afisa Maendeleo Ya Jamii Msaidizi Daraja La II, Tabibu Daraja La II, Mteknolojia Maabara II, Mfamasia Daraja La II, Daktari Daraja La II, Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja La II, Legal Officer II.

Related Posts