Maalim Seif  Kuombewa Dua Leo  – Global Publishers



“Ndugu wananchi wa Zanzibar na Watanzania kwa ujumla, kwa masikitiko makubwa nakujulisheni leo tarehe 17 Februari, 2021, majira ya saa tano asubuhi, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amefariki dunia.”

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi akitangaza kifo cha Maali Seif, kilichotokea miaka minne iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Jana Februari 16, Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Ismail Jussa Ladhu alitangaza kufanyika kwa dua kumuombea Maalim leo Februari 17 katika Mskiti wa Mkunazini (Unguja), Msikiti wa Mtambweni (Pemba) na Msikiti wa Kichangani, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Aliondoka duniani akiwa ameziacha harakati zake za upinzani zikizidi kumea kwa kasi. Kwa hakika mjadala ungekuwa tofauti kama angefariki wakati ule chama chake cha zamani cha wananchi (CUF) kikiwa katikati ya mgogoro.


Related Posts