Kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji kuondoa adha kwa wakazi laki 450 Butimba

Kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji uliyopo Butimba Jijini Mwanza unakwenda kuondoa adha ya upatikani wa maji kwa kwa wakazi takrabani 450,000 katika wilaya za Nyamagana na Ilemela Jijini Mwanza.

Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mkoa wa Mwanza MWAUWASA, Neli Msuya ameeleza kuwa mradi wa maji wa Butimba umekamilika October 2023, kwa uzalishaji wa maji umeongezeka na kufikia lita milioni 138 kutoka lita milioni 90, zilizokuwa zikizalishwa hapo awali.

Baadhi ya maeneo yaliyoanza kunufaika na mradi huo ni pamoja Buhongwa ambapo awali wakazi wa eneo hilo walikuwa wakipata maji kwa wiki mara moja.

Mara baada ya mradi huo kukamilika kwa 100%, kinachofanyika kwa sasa ni usambazaji wa maji kwa wananchi, kwani tayari MWAUWASA inatekeleza mradi wa ujenzi wa matenki matano yatakayo kuwa na uwezo wa kubeba lita za maji milioni 31, hii itarahisisha kwa kwa wakazi wa maeneo mengi kuwa na uhakika wa maji.

Wizara ya Maji kwa kushirikiana na Benki ya uwekezaji ya Ulaya pamoja na shirika la maendeleo la Ufaransa imekamilisha utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa chanzo za maji Butimba kwa gharama ya Euro milioni 31.17, sawa na shilingi bilioni 71.

Ujenzi wa mradi mkubwa wa maji wa Butimba Jijini Mwanza ulianza kutekelezwa February 2021, na umekamilika October 2023.

Related Posts