Mvua ilivyofunga maduka Njombe | Mwananchi

Njombe. Ikiwa imepita siku moja, Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) kutangaza kuwepo kwa Mvua katika Mikoa 15 ukiwemo Mkoa wa Njombe, Hali hiyo imejitokeza kuanzia majira ya saa 8.00 mchana na kudumu kwa zaidi ya masaa mawili.

Mvua hiyo ambayo iliambatana na upepo mkali na ngurumo za radi kiasi cha kufanya baadhi ya maduka wafanyabiashara  kufunga maduka kwa muda ili maji yasiweze kuingia ndani.

Mvua hiyo imeathiri shughuli za kiuchumi ikiwepo huduma za kijamii kwa wananchi kutoka sehemu moja kwenda nyingine kutokana na kuwepo kwa upepo mkali na ngurumo za radi.

Mwananchi Digital imetembelea katika baadhi ya maeneo na kuzungumza na madereva bodaboda kuhusiana na athari waliyoipata.

Dereva boda boda Michael Nicholas amesema kwa upande wao endapo mvua hii itanyesha muda wote italeta athari katika biashara yao kwa kushindwa kubeba wateja wakihofia kuloana.

Amesema hata kwa wakulima pia inaweza kuleta madhara kama mvua ikizidi sana huenda mazao yanaweza kuharibika na kusababisha hasara kutokana na uwekezaji wao katika kununua mbegu na mbolea.

“Kwasisi boda boda itabidi tubadili ratiba kama itaanza mchana kama leo kazi tutafanya asubuhi lakini ikinyesha muda wote kwetu itakuwa majanga” amesema Nicholas.

Mmoja wa wafanyabiashara wa bidhaa za majumbani Shime Gwishi  amesema amelazimika kufunga duka ili kuepuka madhara ikiwepo maji kujaa ndani na ngurumo za radi.

“Nimeona ni vyema nirudishe duka kwani hata nikiendelea kukomaa kuuza wateja wanatoka wapi ?huku tayari mvua kubwa imetanda kila eneo,”amesema.Gwisha.

Related Posts