Unguja. Wizara ya Maendeleo ya Makazi ipo katika hatua za kutafuta wawekezaji watakaowezesha ujenzi wa kisasa katika maeneo ya Kilimani, Kikwajuni na Michenzani na kubomoa majengo yaliyopo ya zamani ili Zanzibar iwe miongoni mwa miji inayotambulika kutokana na usanifu wa majengo ya kisasa na yenye mvuto.
Majengo hayo yalijengwa na Rais wa Awamu ya Kwanza, Abeid Amani Karume baada ya Mapinduzi mwaka 1964.
Hayo yamebainika katika mkutano wa 18 wa Baraza la Wawakilishi Chukwani leo Alhamisi Februari 20, 2025.
Hayo yalibainishwa baada ya mwakilishi wa Mwanakwerekwe Ameir Abdalla Ameir kutaka kufahamu mpango mkakati wa kuzijenga nyumba za kisasa za makazi katika maeneo hayo kutokana na uchakavu wake.
Akitoa ufafanuzi wa hoja hiyo, Naibu waziri huyo amesema majengo hayo yaliyopo katika maeneo hayo yatavunjwa na kujengewa mapya yatakayobeba watu wengi zaidi kwani muda wa majengo hayo umeisha.
“Serikali ipo katika hatua za kutafuta wawekezaji mbalimbali watakaowezesha ujenzi wa nyumba za kisasa katika maeneo ya Kilimani, Kikwajuni na Michenzani kwa kuyavunja majengo yaliopo na kujenga mapya yatakayobeba watu wengi zaidi kwani muda wa kuishi majengo hayo umeisha,” amesema Salha.
Pia, Wizara hiyo kupitia kampuni ya Infinit kutoka Dubai ipo katika mazungumzo na mwekezaji huyo ambayo imeonesha nia ya kuwekeza katika eneo la Kikwajuni na hatua za awali za michoro ya usanifu wa majengo katika eneo hilo imewasilishwa.
Serikali itakamilisha mpango huo kwa kuingia ubia na wawekezaji kwa mujibu wa taratibu ili kufanikisha ujenzi huo pamoja na mikopo nafuu baina ya Serikali na wekezaji ikiwemo (EPC + Finance) ili kufanikisha mpango huo kwa muda