DKT. TULIA AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI YA MKUTANO WA 6 WA IPU

Rais wa Umoja wa Mabunge
Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Tulia Ackson, ameongoza Kikao cha kwanza cha Kamati ya kuratibu Maandalizi ya
Mkutano wa 6 wa Maspika wa Mabunge Duniani leo tarehe 16 Mei, 2024 Geneva nchini
Uswisi.

Kikao hicho kilichohusisha
Maspika Wawakilishi kutoka Mabunge ya Kanda 6 za Kisiasa na Kijiographia,
Wawakilishi kutoka Kamati ya Uongozi, Viongozi wa Makundi ya Wanawake na Vijana
pamoja ya Uongozi wa Umoja huo kimejadili kuhusu mapendekezo ya ajenda za
Mkutano huo wa Maspika unaotarajiwa kufanyika mwakani na kuona namna changamoto
za sasa zinazoikumba Dunia zinavyoweza kuwa sehemu ya ajenda za Mkutano huo.

Baadhi ya changamoto
zinazotarajiwa kujadiliwa ni pamoja na Mabadiliko ya tabianchi, ukame na njaa
hususani Sub Saharan Afrika, machafuko ya amani na vita zinazoendelea  katika baadhi ya mataifa Duniani, usawa wa
kijinsia na kujenga Jumuiya jumuishi na za ushilikishwaji. Aidha, mjadala wa
demokrasia na matumizi ya akili bandia na matokeo yake nayo ni sehemu ya ajenda
zinazotarajiwa.

Rais wa Umoja wa Mabunge
Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.
Tulia Ackson, akiongoza Kikao cha kwanza cha Kamati ya kuratibu Maandalizi ya
Mkutano wa 6 wa Maspika wa Mabunge Duniani leo tarehe 16 Mei, 2024 Geneva
nchini Uswisi. (Kushoto ni Katibu Mkuu wa IPU Ndg. Martin Chungong).


 

Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, akiongoza Kikao cha kwanza cha Kamati ya kuratibu Maandalizi ya Mkutano wa 6 wa Maspika wa Mabunge Duniani leo tarehe 16 Mei, 2024 Geneva nchini Uswisi.

Related Posts