Msingi wa utafiti huo ni kuwa kabichi ina madini maarufu kama fibre, asidi na vitamini ambayo yanasaidia kupunguza mafuta mengi ndani ya mwili wa mwanamume.
Kula kabichi mara tatu kwa siku kunapunguza unene kupita kiasi miongoni mwa wanaume, wanasayansi wamebaini.
Katika utafiti uliochapishwa kwenye jarida la BMJ Open, kabichi iliyotiwa chumvi, kuchachuka na pia kuongezewa viungo vingine kama vitunguu, husaidia kupunguza unene.
Msingi wa utafiti huo ni kuwa kabichi ina madini maarufu kama fibre, asidi na vitamini ambayo yanasaidia kupunguza mafuta mengi ndani ya mwili wa mwanamume.
Unene kupita kiasi hutokana na kula vyakula ambavyo huongeza nguvu na mafuta mwilini. Vyakula hivyo ni kama ugali, wali, vyakula vya protini, madini yenye chumvi na pia mafuta.
Utafiti huo ulishirikisha wale watu ambao walikula kabeji siku moja na wale ambao walikula chakula hicho mara tatu kwa siku.
Ilibainika waliokula kabichi yenye uchachu mara tatu walipunguza unene huku waliokula kabeji mara moja wakipunguza japo kwa kiwango cha chini.
Kwa upande mwingine, waliokuwa na unene na hawakula kabichi, waliendelea kuandamwa na uzani wa juu. Kwa hivyo, utafiti huo uliweka bayana kuwa kula kabichi kwa njia moja au nyingine, kunasaidia kupunguza unene ambao unaendelea kuwa kati ya matatizo ya kiafya ya kutisha ulimwenguni.
Hata hivyo, kuna madai kuwa uwepo wa chumvi nyingi katika kabichi ni hatari kwa afya. Lakini, uwepo wa madini ya chumvi (potassium) katika kabichi hiyohiyo yenye uchachu, kunalezwa kuwa husaidia mno.
(Makala haya awali yalichapishwa katika tovuti ya gazeti dada la Taifa Leo)