Wawakilishi saba wa LBL mbaroni Geita

Geita. Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linawashikilia watu saba ambao ni wawakilishi wa Kampuni ya Leo Beneth London (LBL) kwa tuhuma za kuendesha biashara ya fedha mtandaoni bila kuwa na kibali cha Benki Kuu ya Tanzania.

Kaimu Kamanda Maro amesema watu hao waliopo mji mdogo wa Katoro wamekuwa wakiwatoza wananchi fedha kati ya Sh50,000 hadi 540,000, wakiwataka watazame video fupi inayotangaza faida watakayokuwa wakipata pindi wakijiunga na kampuni hiyo, jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Waliokamatwa ni Juma Nicholaus, Stefano Kafulila, Ramadhan Masood, Alfred Matiba, Rebeca Mazabali, Elizabeth Zacharia na Athuman Masunga.

Jeshi hilo, pia, limekamata vifaa mbalimbali vilivyokuwa vikitumika kutekeleza uhalifu huo ambavyo ni kompyuta moja, simu janja nane, laini za simu 21, notebook yenye majina na nyaraka mbalimbali ambazo zinakumbukumbu za wateja.

Amesema uchunguzi umebaini umebaini kampuni ya LBL haina nyaraka halali za kufanya biashara za fedha wala kuchangisha wananchi na pia hana vibali kutoka BOT kwa ajili ya kufanya biashara hiyo na kwamba watu hao wanaendelea kushikiliwa kwa taratibu za kufikishwa mahakamani.

Related Posts