ZIKIWA zimesalia siku mbili ili kuchezwa Mzizima dabi, kocha wa Azam Rachid Taoussi ajitanua kifua mbele kwa Simba akisema kikosi chake hakina sababu za kufungwa na Wekundu wa Msimbazi.
Azam ambayo iko nafasi ya tatu katika ligi, ikiwa imecheza mechi 20 ikivuna jumla ya alama 43, huku mchezo wa mwisho wakitoka na suluhu dhidi ya Coastal Union.
Azam imecheza mechi 20, huku ikicheza ugenini michezo tisa, ikishinda na kutoka suluhu mara tatu kila mmoja,ikipoteza miwili na sare moja.
Huku nyumbani ikicheza mechi 11, ikishinda tisa, suluhu moja na kufungwa moja. hesabu zinazokamilisha michezo 20 kati ya 30 ya msimu huu.

Akizungumza na Mwanaspoti kocha huyo alisema kuwa,mchezo dhidi ya Simba utaamuliwa na wachezaji wake.
Alisema kuwa, mchezo wowote unaamuliwa na wachezaji kwa kuchagua kujituma au kulegea kwani kazi yake kama mwalimu aliishaikamilisha.
“Mastaa wangu wanajua kabisa wanachotakiwa kufanya na ni kushinda ili wabaki kwenye mbio za ubingwa au wapoteze ili kujiweka kwenye mazingira magumu ya michuano.
“Wana kila sababu ya kupata ushindi dhidi ya Simba, kwani Azam sio timu inayotakiwa kuwa nyuma ya hizo klabu mbili kongwe nchini, kutokana na uwekezaji waliofanya.
Aliongeza kuwa;”Azam sio timu inavyotakiwa kupoteza mara mbili mfululizo nyumbani na ugenini, haiwezekani kabisa.”
Huu ni mchezo wa pili kwa msimu huu, huku wa kwanza Azam ikitoka na kilio cha kupigwa mabao 2-0 na kudondosha alama tatu.
Simba inayoshika nafasi ya pili katika ligi imeizidi Azam alama saba, huku ikiwa imecheza mechi 19 mpaka sasa.
Wekundu hao wataikaribisha Azam katika Uwanja wake wa nyumbani KMC Complex, Jumatatu Februari 24 Saa 10:00 Jioni.
Rekodi zinaonyesha kuwa timu hizi zimeanza kukutana tangu mwaka 2008, lakini misimu sita iliyopita, bado Azam imekuwa haina kiwango kizuri mbele ya Simba

MISIMU MITANO AZAM VS SIMBA