WANANCHI MNAOTAPELIWA KUPITIA MTANDAO YA SIMU TOENI TAARIFA KWA MAMLAKA HUSIKA-WAZIRI SILAA

Na Pamela Mollel,Arusha

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya habari,Jerry Silaa amewataka wananchi wanaotapelewa kwa njia ya mitandao ya simu kutoa taarifaa katika mamlaka husika ili hatua kali zaidi zichukuliwe ili kukomesha utapeli huo

Alitoa rai hiyo jijini Arusha Februari 21,2025 katika mkutano maalumu na waandishi wa habari kuhusu kampeni kabambe ya “SITAPELIKI “inayolenga kutoa elimu kwa jamii

Waziri Silaa anasema wananchi wanaotapeliwa watoe taarifaa zao kwa Jeshi la polisi lakini pia kwa Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)

“Endapo wananchi watatoa taarifaa polisi mamlaka husika itafanya jitihada za kawasaka matapeli wanaofanya utapeli kupitia simu

Pia amesisitiza kwa wadau wote wa vyombo vya habari kushiriki katika utoaji wa elimu kwa jamii juu ya kampeni ya “SITAPELIKI” ambayo ni kampeni endelevu itakayokwenda kudhibiti vitendo vya utapeli na ulaghai kupitia mitandao.

 

Related Posts