Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama leo Februari 22, 2025 amefanya ziara ya kukagua miundombinu pamoja na huduma zinazotolewa katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni (Mkata) Mkoani Tanga inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi kesho Februari 23, 2025 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Miongoni mwa wodi alizotembelea na kuzikagua Waziri Mhagama ni pamoja na wodi ya wazazi, mama na mtoto, wodi ya watoto wachanga, wodi ya huduma za dharura pamoja na huduma zinazotolewa katika jengo la wagonjwa wa nje (OPD).
Waziri Mhagama ameambatana na timu kutoka Wizara ya Afya akiwemo, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Dkt. Hamad Nyembea pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Tumainiel Macha.