PROF MBALAWA AITAKA ATCL KUTOA HUDUMA BORA NA WAKATI..

NA DENIS MLOWE, IRINGA

WAZIRI wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amelitaka shirika la ndege nchini kuhakikisha safari za ndege za shirika hilo zinafanyika kwa ratiba inayoeleweka na kuondokana suala zima la kuchelewa na kutoa huduma kwa ubora makini kwa abiria wake.

Prof. Mbarawa ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa safari za ndege la shirika hilo kutoka Dar es Salaam kwends Iringa baada ya miaka 8 tangu kusitisha safari hizo na kuzinduliwa tena na kuonyesha mafanikio makubwa kwa kuwa na abiria wengi tofauti na uzinduzi wa mikoa mingine ambapo huwa asilimia 60 tofauti na Iringa ambapo asilimia 100 kwa siku kwa kujaza abiria kuja na kurudi.

Kutokana hilo Prof Mbalawa amemwigiza mkurugenzi wa shirika la ndege Tanzania Injinia Peter Ulanga kuangalia namba za watu wanaosafiri na ndege Iringa kwenda Dar es Salaam na kutoka Dar es Salaam kurudi Iringa katika ruti zake kama abiria wataongezeka zaidi basi waongeze ruti zaidi kwa wiki.

Alisema kuwa katika uzinduzi wa leo asilimia 100 ya ndege imejaa hali ambayo ni tofauti kwenye uzinduzi wa safari za ndege katika mikoa mingine kuwa na asilimia 60 hivyo Iringa iangaliwe kwa upendeleo katika kuongeza safari zake tofauti na sasa ambazo ni ruti tatu kwa wiki.

Aidha alitoa ushauri endapo uwanja utakamilika kwa asilimia 100 katika uwekaji wa Taa basi wafikiria pia Kuwe na ruti ya usiku ndani ya mkoa iringa na mikoa mingine kama Dodoma kwenda Dar na maeneo mengine.

Alisema kuwa shirika Atcl linahitaji kukuza ukubwa wa biashara yake kwa kuzingatia ubora wa huduma na kuwataka kusimamia kwa weledi na ubunifu ili kiweze kudumu katka soko la usafarishaji wa anga.

“Simamieni utendaji wa kazi ili kampuni iwe na tija kuinua uchumi wa nchi hivyo ujuzi wa kutosha katika kazi unahitajika.” Alisema

Mbalawa aliwaagiza ATCL kuhakikisha wanashughulikia malalamiko ya wateja haraka ili kuendana na soko kuliko mteja wiki nzima hajashughulikiwa changamoto yake na kutoa ushauri kuhakikisha Shirika linaweka bei inayolingana na huduma zinazotolewa na ndege.

Alitoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha uwanja wa ndege Nduli umekamilika kwa asikimia 95 hali kwa kutoa zaidi ya bilioni 7 katika kukarabati uwanja huo.

Kwa upande wake Mkurugenzi ATCL, Injinia Peter Ulanga alisema kuwa ndege shirika hilo litafanya ruti zaidi 3 kwa wiki na nauli ya sh. 199,200 kwenda na kurudi inajumuisha usafirishaji wa mzigo wenye uzito wa hadi kilo 23 kwa sehemu ya mizigo, pamoja na begi la mkononi lisilozidi kilo saba, bila malipo ya ziada.

“ATCL itaanza na safari tatu kwa wiki, kila Jumatatu, Jumatano na Ijumaa ambapo wanachama wa Twiga (Twiga Members) wataweza kulipia tiketi kwa kutumia pointi zao za safari,” ilisema

Alisema kurejeshwa safari hizo zitakazotumia dk 59 hadi kufika itachochea idadi ya watalii wanaotembelea mkoani Iringa kuongezeka na kuwezesha wafanyabiashara kuondokana na kuchelewa katika kusafirisha mizigo yao.


 

Related Posts